Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Mahusiano na Uratibu Dkt. Mary Nagu akizungumza na watumishi wa Ofisi ya Rais Tume ya Mipango alipotembelea Tume hiyo leo jijini Dar es salaam na kupewa taarifa ya namna inavyofanya kazi na mipango waliyonayo ili kufikia uchumi wa kati ifikapo 2025 kulingana na sera ya taifa.
Katibu Mtendaji wa Ofisi ya Rais Tume ya Mipango Dkt. Philip Mpango akitoa taarifa kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Mahusiano na Uratibu Dkt. Mary Nagu alipotembelea Tume hiyo leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya viongozi wa Ofisi ya Rais Tume ya Mipango wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Mahusiano na Uratibu Dkt. Mary Nagu alipotembelea Tume hiyo leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya watumishi wa Ofisi ya Rais Tume ya Mipango wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Mahusiano na Uratibu Dkt. Mary Nagu alipotembelea Tume hiyo leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya watumishi wa Ofisi ya Rais Tume ya Mipango wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Mahusiano na Uratibu Dkt. Mary Nagu alipotembelea Tume hiyo leo jijini Dar es Salaam.
Na Happy Shirima – Maelezo-Dar
16.2.2015.
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais Mahusiano na Uratibu Mh. Dkt.Mary Nagu amewaagiza watumishi wa Ofisi ya Rais Tume ya Mipango kujituma na kufanya kazi kwa bidii ili kufanikisha na kufikia Dira ya Maendeleo ya Taifa ya mwaka 2025.
Waziri Nagu ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na wafanyakazi wa Ofisi ya Rais Tume ya Mipango ambapo amewaagiza kujituma zaidi kwenye tafiti mbalimbali zikiwemo za kiuchumi na kijamii ili kusaidia kukuza uchumi wa nchi na kupunguza umaskini kwa wananchi.
Amesisitiza kuwa Tume hiyo inawajubu wa kusimamia na kupanga mipango itakayoenda sanjari na ongezeko la idadi ya watu ili kupunguza kasi ya umaskini nchini kwa kuzingatia uzazi wa mpango utakaoendana na mipango imara ya kukuza uchumi.
“Nchi yetu inarasilimali nyingi na hivyo kuna fursa nyingi na na zitumike vizuri kwa njia za kisasa kama ukuzaji wa viwanda ambavyo vinasaidia upatikanaji wa ajira na kuona uchumi unatengamaa”alisema Dkt.Nagu.
Naye Katibu Mtendaji Ofisi ya Raisi Tume ya Mipango Dkt. Philip Mpango amesema kuwa ofisi hiyo inakabiliwa na changamoto mbalimbali kama ukosefu wa fedha, idadi ndogo ya wataalamu na uchakavu wa jengo.
Tume ya Mipango ina jumla ya watumishi 151, ambapo wanawake idadi yao ni 60 na wanaume 91 mabao wanafanyakazi kwa bidii na kuipenda nchi yao katika kuiletea maendeleo endelevu kwa watu wake.
Hata hivyo Katibu Mpango amesema kuwa ofisi hiyo inaratibu utekelezaji wa mipango ya Taifa na Mapendekezo ya mipango ya maendeleo kwa mwaka 2016 2017.
No comments:
Post a Comment