Wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni wa Serikali za Mitaa (LAPF), wakishangilia wakati walipokuwa wakiingia kwenye viwanja vya Shule ya Dodoma Sekondari walipokutana kwa ajili ya michezo ya Bonanza la kuukaribisha mwaka mpya wa 2015, mjini Dodoma jana.
Wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni ya Serikali za Mitaa (LAPF), wakishindana kufukuza kuku wakati wa Bonanza la wafanyakazi hao, toka kanda ya Ziwa, Kanda ya Kaskazini na Kanda ya Kati walipokuwa wakiukaribisha mwaka mpya, mjini Dodoma jana.
Wafanyakazi wa LAPF wakimenyana katika mchezo wa Netboli walipokuwa kwenye Bonanza kabla ya kukutana kwanye hafla ya kuukaribisha mwaka mpya wa 2015.
Wafanyakazi wa LAPF Kanda ya Ziwa na Makao Makuu, wakipigana kumbo kwenye mchezo wa mpira wa miguu walipokuwa kwenye Bonanza la kuukaribisha mwaka mpya ambapo wafanyakazi wa Makao Makuu, walishinda mabao 5-1 mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Shule ya Dodoma Sekondari.
Wafanyakazi wa LAPF, wakiwa katika mchezo wa kuvuta kamba. (Picha zote na John Banda)



No comments:
Post a Comment