TANGAZO


Thursday, January 29, 2015

Wanawake wakerwa na mauaji Misri

Maandamano Misri
Zaidi ya wanawake 100 wa Misri wameandamana mjini Cairo, kutaka uchunguzi ufanywe dhidi ya mauaji ya mkereketwa mmoja wa haki za kibinadamu, Shaimaa Sabbagh.
Mkereketwa huyo aliuwauwa wakati wa maadhimisho ya maandamano ya mapinduzi ya kiraia Nchini humo mnamo mwa 2011.
Wanawalaumu walinda usalama kwa kumpiga risasi mkereketwa huyo aliyekuwa na umri wa miaka 32 na ambaye hakuwa amejihami.
Mkereketwa huyo aliuuwawa mwishoni mwa juma lililopita.
Picha ya Shaimaa Sabbagh akifariki iliibua hasira kubwa nje na ndani ya Misri.
Kifo chake pia kiliibua ukosoaji mkubwa dhidi ya polisi na wakuu wa gazeti la serikali la, Al Ahram.

No comments:

Post a Comment