Afisa Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Amina Sanga akiwaelimisha vijana wa Wilaya ya Kyela kuhusu mwongozo unaosimamia Mfuko wa Maendeleo ya Vijana wakati wa semina ya Ujasiriamali, Stadi za Maisha, Ujuzi na Mfuko wa Maendeleo ya Vijana iliyofanyika jana katika Wilaya ya Kyela Mkoa wa Mbeya.
Vijana wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyela Mkoa wa Mbeya walioudhuria semina ya Ujasiriamali, Stadi za Maisha, Ujuzi na Mfuko wa Maendeleo ya Vijana wakifuatilia mambo mbalimbali yaliyokua yakiendelea wakati wa semina hiyo.
Mwenyekiti wa Wadau
Self Supporting Group Bw. Godbless Konga wanne kulia akizungumza na maafisa
kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo walipotembelea kikundi
hicho kuangalia mradi unaoendeshwa na vijana wa kikundi hicho jana wakati wa
ziara ya kukagua miradi ya vijana wa Wilaya ya Kyela Mkoa wa Mbeya. (Picha
zote na: Genofeva Matemu – Maelezo)
Na Genofeva Matemu
Tarehe: 29/01/2014
VIJANA wa Halmashauri
ya Wilaya ya Kyela wameshauriwa kuachana na fikra potofu za kusubiria kuajiriwa
na serikali mara tu wanapomaliza elimu ya chuo kikuu bali kutumia ujuzi
walioupata kujiajiri wenyewe na kutoa fursa kwa vijana wengine ambao hawakupata
fursa ya kujiendeleza.
Rai hiyo imetolewa na
Mkuu wa Wilaya ya Kyela Bibi Magreth E. Malenga alipokua akizungumza na wadau
wa vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo walipofika
ofisini kwake kabla ya kukutana na Vijana wa Wilaya hiyo kwa ajili ya kutoa
elimu ya Ujasiriamali, Stadi za Maisha, Ujuzi, na Mfuko wa Maendeleo ya Vijana
jana katika Wilaya ya Kyela Mkoa wa Mbeya.
Akizungumza na wadau
hao Bibi Malenga amesema kuwa amefurahishwa na ujio wa wadau kutoka Wizara ya
Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kwani anaamini kuwa ujio huo utawasaidia vijana
wa Kyela kujitambua na kupata mbinu mbalimbali za kiujasiriamali ili waweze
kujitegemea.
“Vijana wa sasa
hawapendi kujiajiri wanapomaliza elimu ya chuo kikuu wanabaki mitahani
wakiilalamikia serikali haitaki kuwaajiri, naamini kwa semina hii vijana wa
Kyela watajitambua na kutumia elimu waliyoipata kuibua miradi mbalimbali itakayowaingizia
kipato” alisema Bibi Malenga.
Kwa upande wake Afisa
Maendeleo ya Vijana Bi. Amina Sanga amewataka vijana wa Kyela kutumia fursa
mbalimbali zilizopo katika Wilaya hiyo kwani kwa kufanya hivyo watakua wameweza
kujiendeleza na kujitegemea hivyo kuondokana na dhana ya kuwa tegemezi katika
jamii.
Naye mwenyekiti wa
kikundi cha vijana kijulikanacho kwa jina la Wadau Self Supporting Group Bw.
Godbless Konga amesema kuwa vijana wa Kyela walikua na ufikiri mdogo katika
masuala ya aunzishaji na usimamiaji wa shughuli ndogondogo kutokana na kutokuwa
na mbinu za kibiashara lakini kutokana na eimu waliyoipata anaamini kuwa vijana watawekeza na kuachana na
dhana ya kuwa tegemezi katika jamii.
Bw. Konga amewataka
vijana wote nchini kuwa wabunifu na kujaribu kuanzisha miradi mbalimbali kwa
kutumia mbinu za kibiashara zitakazowakwamua kimaisha ili kuachana na tabia ya
kuitegemea serikali kwa kila jambo.






No comments:
Post a Comment