Kaimu Mkurugenzi
Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo Bibi Nuru Mwendapole kushoto akizungumza na
Mwezeshaji kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi Ester
Riwa jana wakati wa ziara ya kutembelea Wilaya hiyo kwa ajili ya kutoa elimu ya
Ujasiriamali, Ujuzi, Stadi za Maisha na Mfuko wa Maendeleo ya Vijana kwa vijana
wa Wilaya ya Busokelo Mkoa wa Mbeya.
Mwezeshaji kutoka
Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi Ester Riwa akiwasisitizia vijana
wa Wilaya ya Busokelo umuhimu wa kuijua Sera ya Maendeleo ya Vijana jana wakati
wa semina ya Ujasiriamali, Stadi za Maisha, Ujuzi na Mfuko wa Maendeleo ya
Vijana iliyofanyika katika Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo Mkoa wa Mbeya.
Maafisa kutoka Wizara
ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo wakimsikiliza kwa makini kijana kutoka
kikundi cha Vijana Maendeleo wanaofuga samaki wakati wa ziara ya kutembelea
vikundi vya vijana wa Wilaya ya Busokelo Mkoa wa Mbeya.
Samaki wakionekana kwa
mbali katika bwawa la samaki linalomilikiwa na kikundi cha Vijana cha Maendeleo
kilichopo Wilaya ya Busokelo Mkoa wa Mbeya.
Kutoka kulia ni Mwezeshaji
kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi Ester Riwa, Afisa
Vijana Mkoa wa Mbeya Bw. George Mbijima, Afisa Maendeleo ya Vijana Bi. Amina
Sanga na Mkuu wa Kituo cha Vijana Sasanda Mbeya Bw. Laurean Masele wakiangalia
nguruwe wa kikundi cha Search Group
Wilaya ya Busokelo walipowatembelea kuangalia shughuli zinazofanywa na kikundi
hicho. (Picha
zote na Genofeva Matemu – Maelezo. Busokelo, Mbeya)
No comments:
Post a Comment