SERIKALI imeendelea kuboresha mazingira ya utoaji wa Elimu ya watu wazima nchini kote wakiwemo wanawake kwa
mkoa wa Mwanza chini ya sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014 .
Akijibu
swali la Mbunge wa viti maalum mhe. Leticia Nyerere, kuhusu asilimia ndogo ya wanawake wasomi kwa mkoa wa
Mwanza ukilinganishwa na mkoa wa Kilimanjaro ambapo Waziri wa Elimu na Mafunzo ya ufundi Dkt. Shukuru Kawambwa alieleza tofauti hiyo inatokana na hali ya
kiuchumi na kijamii.
Aidha
mhe.Kawambwa ameeleza mpaka sasa
serikali imeanzisha pogramu mbalimbali
ikiwemo ya Ndiyo Ninaweza katika wilaya 9 ikiwemo ile ya Ilemela
Mwanza,ambapo hutoa mafunzo yake kwa njia ya kieletronic pamoja na Mpango wa uwiano kati ya Elimu ya
Watu Wazima na Jamii ijulikanayo kama MUKEJA.
“Serikali
imechukua hatua mbalimbali kuhakikisha kuwa wananchi wote wakiwemo wanawake
wanapata elimu ambayo ni haki yao ya msingi ili kuweza kuwasaidia katika
shuguli zao za kila siku za maendeleo” alisema Dkt.Kawambwa.
Aliongeza
kuwa ni jukumu la Wizara, Mikoa na
Halmashauri kuhamasisha wananchi kujiunga na program hizo ili kujifunza
kuandika,kusoma na kuhesabu kwa manufaa yao na jamii inayowazunguka.
Kulingana
na ripoti ya sense ya watu na makazi ya
mwaka 2014 iliyofanyika mwaka 2012
ambapo inaeleza asilimia 24.5 ya wanawake wenye umri wa miaka chini ya 15 na
zaidi katika mkoa wa Mwanza hawajui kusoma na kuandika ukilinganisha na mkoa wa
Kilimanjaro wenye asilimia 9.7 wakati Dar es Salaam ni asilimia 5.2.


No comments:
Post a Comment