![]() |
| Naibu Waziri Nkamia |
Hayo yalisemwa na Naibu
Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Juma Nkamia alipokuwa akijibu swali la Mhe.
Muhammad Sanya kuhusu bei ya magazeti
kuwa juu na hivyo kupelekea wananchi kukosa taarifa muhimu.
Mhe. Nkamia alikiri
kuwa ni kweli bei za magazeti nchini ni kubwa na hiyo inatokana na gharama
kubwa za uzalishaji, uendeshaji pamoja na usambazaji, hivyo vyombo vya habari vya kijamii vitakuwa
mbadala mzuri wa wananchi kupata habari.
“Ni vizuri halmashauri
zikaanzisha vyombo vya habari vya kijamii ili kurahisisha upataikanaji wa
habari kwa wananchi hususani wale walioko vijijini ambao wengi wao hutegemea
vyombo hivyo kupata taarifa” alisema Nkamia.
Alisema iadha vyombo vya habari vya kijamii husaidia
sana kutoa taarifa muhimu kwa jamii
husika kwa wakati bila ya kujali faida kwa kufuata taratibu na sheria za
utangazaji zilizowekwa na serikali.
Pia aliwaomba waandishi
wa habari wazingatie maadili ya kazi zao ili kuepusha kufungiwa kwa magazeti
pale inapoonekana vyombo hivyo vimekiuka na kwenda kinyume na sheria na taratibu
zinazosimamia vyombo vya habari nchini.


No comments:
Post a Comment