Mwanasheria Mkuu wa Serikali Jaji George Masaju akitoa ushauri kwa Bunge la Jamhuri.
Mbungge wa Kawe, Halima Mdee akitoa mchango wakati
wa kujadili taarifa za kamati za Bunge, bungeni mjini Dodoma. (Picha
zote na Hussein Makame, MAELEZO, Dodoma)
Usafiri wa Reli Kuboreshwa
Na
Lorietha Laurence-Maelezo Dodoma
SERIKALI imejipanga
katika kuboresha usafiri wa reli ya kati ili kuondoa adha ya usafiri kwa wananchi wa
ukanda huo.
Akijibu hoja za wabunge
kujadili taarifa ya kamati ya miundo mbinu mjini Dodoma Waziri wa Uchukuzi mhe.
Samweli Sitta ameeleza kuwa ujenzi wa reli ya kati unatazamiwa kuanza hivi
karibuni kwa hatua ya standard geji.
Aidha aliongeza kwa
upande wa reli ya Tanga ,Arusha na
Musoma usanifu wa ujenzi umeshakamilika, pamoja na reli ya Mtwara kwenda mbambabei ambao nao upo
mbioni kuanza.
“Usafiri wa reli ni
muhimu sana kwa nchi yetu huu hivyo
serikali inahakikisha kuwa inaboresha usafiri huo ambao unatumiwa na watu wengi ” alisema
Mhe. Sitta.
Pia kwa upande wa
reli ya Dar es Salaam uboreshwaji unatarajiwa kuanza kwa kushirikiana na wadau
kutoka ujerumani kwa kupanua usafiri huo mpaka maeneo ya Pugu na kuwafikia watu wengi .
Alizidi kufafanua kuwa
kuna miradi mbalimbali inayofanywa na
serikali kwa jiji hilo kwa madhumuni ya kupunguza msongamano wa foleni, ikiwemo
mradi wa Tazara Flyover,Daraja la Kigamboni, daraja la Surrender bridge II,
Ubungo fly over ,mabasi yaendayo kasi na upanuzi wa bandari ya Dare s Salaam.
Naye Waziri wa
Fedha mhe. Saada Mkuya amesisitiza kuwa Tanzania iweze kujisimamia kwa kutumia
vyanzo vyake vya fedha ili kuhimiza utendaji wa kazi za ndani ikiwemo
kuimarisha sekta ya uchukuzi.
Bunge laridhishwa na utendaji wa serikali
Na Hussein Makeme, MAELEZO, Dodoma
KAMATI za Bunge za Serikali za Mitaa (LAAC) na ile
ya Hesabu za Serikali (PAC), zimeridhishwa na mafanikio na hatua
zilizochukuliwa na Serikali kwa kuongeza mapato yake na kushughulikia
changamoto zinazoikabili katika kutekelza majukumu yake.
Kufuatia hali hiyo, Bunge limepitisha taarifa za kamati
hizo na nyingine tatu, huku Serikali ikiahidi kufanyia kazi yale yote
yaliyopendekezwa kwenye taarifa hizo ili kulipeleka Taifa kule kunakotakiwa.
Taarifa za Kamati ambazo Bunge limezipitishwa jana
na juzi usiku ni za Kamati ya Bajeti, Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC),
Hesabu za Serikali (PAC), Miundombinu na Nishati na Madini.
Akihitimisha hoja yake, Mwenyekiti wa Kamati ya LAAC,
Rajabu Mbarouk aliipongeza Serikali na Waziri wa TAMISEMI, Hawa Ghasia kwa
hatua alichokua kwa watendaji wa Serikali waliobainika kutumia vibaya fedha za
umma.
“Mimi ni mpinzani lakini kwa hili, kwa kweli
nimpongeza Waziri kwa sababu jana aliniletea list (orodha) karibu ya
halmashauri zote nchini ambazo wakurugenzi amewachukulia hatua, kilichobaki ni
mimi kuichukua ile taarifa na kumpelekea kwa CAG kwa ajili ya kuihathibitisha”
alisema Mbarouk.
Naye Mwenyekiti wa Kamati ya PAC, Zitto Kabwe
aliipongeza Malmalaka ya Bandari Tanzania (TPA) kwa kuongeza mapato na kwamba
wameiomba iongeze mapatao katika miaka ijayo ili kuifanya mamlaka hiyo iwe na
tija kwa taifa.
“Ni lazima tuwe wakweli, Mamlaka ya Bandari
imeongeza sana sana ufanisi katika kazi zake, mapato yameongezeka kutoka
shilingi Bilioni 320 mpaka shilingi Bilioni 537 katika kipindi cha miaka
miwili” alisema Zitto.
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu
Nchemba aliithibitishia kamati na wabunge waliotoa michango yao kuwa wamepokea
michango yao na wataifanyia kazi.
“Kwanza nisema ndugu Mwenyekiti, tumewasikia
wabunge, tumepokea waliyoyasema na tutayafanyia kazi, tupo kwa ajili hiyo”
alisema Naibu Waziri Nchemba.
Alisema tangu mwaka wa fedha ulipoanza, mkakati wa
Wizara chini ya usimamizi wa Waziri wa Fedha ilikuwa ni kuhakikisha kila fedha
inapokusanywa inakwenda pale ilipokusudiwa.
Alifafanua kuwa hata hoja za baadhi ya wabunge kuwa
kuna miradi imepata mgawo sifuri, inawezekana hiyo sifuri ni ya fedha zile
zinazotoka nje.
“Naongea hili kwa uhakika, mwaka wa fedha uliooanza
tu tulitoa Bilioni 500 kwa ajili ya miradi ya maendeleo na mpaka wizara zingine
wakashangaa wakauliza hizi fedha mmekosea au ndivyo kweli zinatakiwa zije”
alisema na kuongeza:
“Walidhani ni za mishahara, haikuzoeleka kutokea
fedha nyingi ndani ya mwezi wa kwanza wa bajeti kwa ajili ya shughuli za
maendeleo”.
Hivyo aliwaomba wabunge wazingatie mambo mamwili,
moja Waziri ameweka utaratibu kwamba kila taasisi inapopokea fedha za maendeleo
ni lazima ipeleke mrejesho imetumia
fedha zile kwa shughul gani na mradi ule uonekane kabla fedha zingine
hazijakwenda.
Alisema jambo la pili ni nia ya Serikali kuhakikisha
kwamba fedha zilizotengwa kwa ajili ya mifuko na matumizi maalum ya miradi ya
maendeleo na kwamba kuanzia mwezi Februari wanarekebisha utaratibu wa
kutengeneza mchanganuo wa fedha kuhakikisha fedha hizo zimekwenda kwenye miradi
ya maendeleo.
Mkutano wa 18 wa Bunge la Jamhuri
unatarajiwa umeahirishwa hadi Jumatatu ambapo bunge hilo linataraji kupokea
taarifa za Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira na Kamati ya Kilimo,
Mifugo na Maji.






No comments:
Post a Comment