TANGAZO


Sunday, December 21, 2014

Somalia yawakataa wanajeshi wa S.Leone

Wanajeshi wa Amisom wakipiga doria katika uwanja wa soka wa Mogadishu .
Wanajeshi wa kulinda amani kutoka Sierra Leone wameondoka nchini Somali na hakuna wanajeshi wengine wa taifa hilo watakaochukua mahala pao kufuatia wasiwasi wa ugonjwa wa Ebola.
Umoja wa Afrika una mpango wa kutafuta wanajeshi wengine kutoka mataifa yenye wanajeshi wake nchini humo.
Zaidi ya wanajeshi 800 wa Sierra Leone walio kusini mwa bandari ya Kismayu wameondoka kuelekea nyumbani.
Walitarajiwa kuondoka mapema lakini safari yao ikacheleweshwa kwa zaidi ya miezi sita baada ya mmoja wa wanajeshi wa Sierra Leone waliotarajiwa kuchukua mahala pao kupatikana na ebola.

No comments:

Post a Comment