Mkurugenzi
Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi
na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues aliposimama kwenye
Kijiji cha Ngeresero kwa ajili ya kuwaungisha wanawake wa kimasai
wanaofanya biashara ya kuuza bidhaa mbalimbali za shanga kwa watalii
wanaosimama kwenye kijiji hicho kwa ajili ya kupata mahitaji mbalimbali,
wakati akielekea kijiji cha Ololosokwan kilichopo wilayani Ngorongoro
mkoani Arusha kukagua miradi mbalimbali inayofadhiliwa na shirika lake
la UNESCO.
Na Mwandishi wetu, Arusha
NDOTO
ya kuwa na kijiji cha dijitali nchini Tanzania itaanza kutimia Januari
mwakani wakati vifaa vinavyotakiwa kukamilisha mradi huo vitakapowasili
kutoka kampuni ya Samsung Electronics.
Kwa
mujibu wa watekelezaji wa mradi huo mkubwa unaotarajiwa kutumia dola za
Marekani milioni 1, Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na
Utamaduni (UNESCO) vifaa hivyo vinatarajiwa kuingia Bandari ya Dar es
Salaam Januari tano mwakani.
Mkataba
wa kuanzishwa kwa kijiji cha dijitali eneo la Ololosokwan tarafa ya
Loliondo wilayani Ngorongoro ulitiwa saini kati ya Unesco na Samsung
electronics Novemba 6 mwaka huu.
Akizungumza
na halmashauri ya kijiji cha Ololosokwan , Mkurugenzi Mkazi wa Shirika
la UNESCO Tanzania, Zulmira Rodrigues amewataka wanakijiji kujiandaa
kwa mabadiliko makubwa ya kijiji chao kinapoingia katika dunia ya
dijitali.
Alisema
mambo ambayo wanastahili kuyaweka sawa ili kufanikisha ndoto zao
kuhakikisha eneo ambalo mitambo na miundombinu ya mradi ipo ni lazima
lisajiliwe kisheria ili kusiwepo na tatizo katika siku za usoni.
Aidha
kutokana na ukubwa wa mashine zinazohusika, hasa makontena ni vyema
wanakijiji wakaangalia maeneo korofi katika barabara za kuelekea huko na
kuzirekebisha, ili magari hayo makubwa yenye vifaa yapite kwa usalama.
Alisema
mradi huo wa miaka mitatu unatarajia kuwawezesha wananchi wa eneo hilo
kuwa na ujasirimali, matumizi ya teknolojia ya kisasa katika mawasiliano
na utafutaji wa masoko, elimu na afya.
Kwa
mujibu wa Bi. Rodrigues kijiji hicho pia kitakuwa na shule iliyoungwa
na mtandao wa kompyuta duniani (intaneti), kliniki ya kisasa, tiba kwa
kutumia teknolojia ya kompyuta na jenereta kubwa linalotumia nishati ya
jua.
Bw.
Abdulaziz Ali wa kitengo cha Transportation and Logistic kutoka UNESCO
akitafsiri bei za bidhaa hizo za kimasai kwa wakimama hao wanaofanya
biashara za urembo wa shanga kwa watalii na wazawa wanaopita katika
kituo kijiji hicho ambapo wengine wao husimama kupata huduma ya chakula
na vinywaji.
Aidha
kuwapo na mtandao wa kompyuta kutawezesha UNESCO kwa kushirikiana na
Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kuanzisha mtaala utakaowawezesha
vijana wa kimasai ambao ni wafugaji kupata elimu wanayoihitaji.
Mwakilishi
huyo wa UNESCO amesema kwamba amefurahishwa na namna watu
walivyoitikia mradi huo ambao umelenga kubadili maisha ya wafugaji hao
kwa kuwawezesha pia kuitumia vilivyo sekta ya utalii.
“Kupitia
mradi huu wananchi wanaweza kujifunza kusoma, kupata maarifa na katika
harakati hizo kujua lugha ya kiingereza ili kuwasaidia kuwa na
mawasiliano na watalii na watu wengine”, alisema Rodrigues.
Mkurugenzi
Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi
na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues akiwasili kwenye kata
ya Ololosokwan kijiji cha Ololosokwan na kupokelewa na Diwani wa kata
hiyo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Irkiramat Foundation (RAMAT) Bw.
Yannick Ndoinyo.
Alisema
ni nia ya Unesco kuhakikisha kwamba inasaidia kufuta ujinga miongoni
mwa wafugaji hao bila kuathiri utamaduni wao wanapoingia katika maisha
ya kisasa.
Kijiji
cha digitali cha Ololosokwan kitakuwa cha nne barani Afrika na yapo
makubaliano ya msingi kwamba kijiji kingine kitajengwa Zanzibar mwakani.
Diwani
wa kata ya Ololosokwan, Bw. Yannick Ndoinyo akiongozana na Mkurugenzi
Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na
Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues aliyefika kijijini hapo
kukagua miradi mbalimbali inayofadhiliwa na shirika la UNESCO pamoja na
kukagua eneo maalum lililotengwa kwa ajili ya kijiji cha digitali cha
Samsung.
Mkurugenzi
Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi
na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues akisalimiana na baadhi
ya kinamama wa mradi wa utalii unaofadhiliwa na shirika la UNESCO kata
ya Ololosokwan kijiji cha Ololosokwan wilayani Ngorongoro mkoani Arusha.
Mkurugenzi
Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi
na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues akizungumza na wakina
mama wa kimasai waliojumuika na waume zao mara baada ya kuwasili
kijijini hapo ambapo aliwaasa kushiriki elimu ya afya ya uzazi wa mpango
ili waweze kuzaa watoto wachache watakaoweza kuwahudumia na aliwaahidi
kuwaanzisha program ya kusoma na kuandika kwa ajili ya kuboresha
mawasiliano yao na watalii wanaotembelea kijiji chao na kununua biashara
zao.
Pichani
juu na chini ni Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa
linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira
Rodrigues akiwaonyesha jambo wakina mama wa kimasai jinsi gani
teknolojia inayvowaleta watu kwa ukaribu zaidi kupitia "Tablet" ambapo
katika kijiji hicho cha digitali cha Samsung wakazi wa eneo hilo watakua
wakipewa mafunzo kutumia kifaa hicho cha "Tablet".
Mkurugenzi
Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi
na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues akifafanua jambo nje
ya maktaba inayofadhiliwa na UNESCO na kuwanufaisha wanafunzi wa shule
ya sekondari Ololosokwani na vijana wa kata hiyo kupanua uelewa zaidi
kwa kusoma vitabu mbalimbali wakati akikagua miradi mbalimbali
inayofadhiliwa na shirika lake. Kushoto ni Diwani wa kata hiyo ambaye
pia ni Mkurugenzi wa Irkiramat Foundation (RAMAT) Bw. Yannick Ndoinyo.
Mkurugenzi
Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi
na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues akiwa kwenye
mazungumzo na viongozi wa juu wa halmashauri ya kijiji wakati wa ziara
yake kijijini hapo mwishoni mwa wiki iliyopita.
Mkurugenzi
Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi
na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues katika picha ya pamoja
na uongozi wa halmashauri ya kijiji cha Ololosokwani mara baada ya
mazungumzo.
Bi.
Zulmira Rodrigues katika picha ya pamoja na baadhi ya wanakijiji wa
kijiji cha Ololosokwan kata ya Ololosokwani wilayani Ngorongoro mkoani
Arusha.
Mkurugenzi
Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi
na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues katika picha ya pamoja
na akina mama wa kimasai wa Kata ya Ololosokwani kijiji cha
Ololosokwani, wilayani Ngorongoro mkoani Arusha mara baada ya kikao
na halmashauri ya kijiji hicho.
Bi. Zulmira Rodrigues akiagana na baadhi ya wakinamama wa kimasai mara baada ya kikao cha halmashauri ya kijiji hicho.
Mkurugenzi
Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi
na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues (kulia) akifafanua
jambo wakati wa kukagua eneo ambalo mitambo na miundombinu ya mradi
itawekwa kwenye sehemu iliyotengwa na halmashauri ya kijiji kwa ajili
ya kijiji cha dijitali cha Samsung. Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa bodi
ya RAMAT, Pokare Koitumet, Diwani wa kata hiyo ambaye pia ni Mkurugenzi
wa Irkiramat Foundation (RAMAT) Bw. Yannick Ndoinyo pamoja na Chifu wa
kijiji cha Ololosokwan kata ya Ololosokwan wilayani Ngorongoro mkoa wa
Arusha.
Muonekano wa eneo hilo huku Bi. Zulmira Rodrigues akiendelea kulikagua.
No comments:
Post a Comment