TANGAZO


Tuesday, December 23, 2014

Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Mahmoud Thabit Kombo afanya ziara katika vituo vya Afya Mkoa wa Kaskaziani 'A' Unguja

Mkuu wa kituo cha Afya cha Mkokotoni Mcha Haji Makame akitoa taarifa kwa Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Mahmoud Thabit Kombo (alievaa miwani) alipofanya ziara ya kutembelea vituo vya afya vya Wilaya Kaskazini A. Wa kwanza (kushoto) mwakilishi wa WHO Zanzibar Dkt. Andymicheel Ghirmany akifuatiwa na mwakilishi wa UNICEF Zanzibar  Bibi Fransisca. (Picha zote na Makame Mshenga-Maelezo, Zanzibar)
Mkuu wa kituo cha Afya Mkokotoni akiwaonyesha  wawakilishi wa UNICEF Bibi Fransisca na mwenzake wa WHO Ghirmany  jiko la kuchoma takataka za Hospitali hiyo.
Wawakilishi wa UNICEF na WHO  wakiangalia takwimu za wagonjwa waliopata matibabu  katika Hospitali kuu ya Wilaya  kwa kipindi cha miezi 11 kunzia Januari  walipofanya ziara na Naibu Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo Wilaya ya Kaskazini A Unguja. 
Daktari dhamana wa Hospitali ya Kivunge  Khamis Hamad akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo na ujumbe aliofuatana nao  walipofanya ziara kuangalia utendaji wa kazi na kujitambulisha.
Mwakilishi wa WHO Zanzibar Dkt. Andymicheel Ghirmany akizungumza na wafanyakazi wa kituo cha afya Chaani  (hawapo pichani) wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Afya Zanzibar  katika vituo vya Wilaya Kaskazini A.
Baadhi ya wafanyakazi wa kituo cha afya cha Chaani  wakimsikiliza Mwakilishi mkaazi wa WHO Zanzibar  wakati wa ziara ya Naibu Waziri kutembelea vituo hivyo.

No comments:

Post a Comment