TANGAZO


Wednesday, December 24, 2014

Magari yazuiliwa Borno msimu huu

Gari lililo shambuliwa mjini Borno
Wenye mamlaka nchini Nigeria katika jimbo la Borno wamezuia harakati za magari nchini humo kuepusha kushambuliwa na kikundi cha Boko Haram.
Amri hiyo imesababisha maelfu ya raia nchini humo kuharakisha kila mmoja kwenda kwenye makazi yake kuhifadhi vyombo hivyo vya usafiri, na amri hiyo inayoanza leo itadumu katika msimu huu wa sikukuu.
Waasi hao wa Boko Haram wamezua wasiwasi mkubwa upande wa kaskazini mwa jimbo la Borno,Yobe na Adamawa .askari hao wa dola ya kiislam wanalenga makanisa wakati huu wa shamra shamra za sikukuu za mwishoni mwa mwaka.
Pengine amri hii inafuatia tukio lililotokea miaka mitatu iliyopita,Ikumbukwe kwamba sherehe za Christimas za mwaka 2011,Boko Haram waliripua kanisa lililoko karibu na mji mkuu wa nchi hiyo,Abuja na kuua watu zaidi ya arobaini

No comments:

Post a Comment