TANGAZO


Wednesday, December 24, 2014

Karama Nyilawila kumvaa Mmalawi

Kushoto ni bondia Said Mbelwa na kulia ni bondia Karama Nyilawila
Bondia wa Tanzania Karama Nyilawila mapema mwakani 2015 ,anatarajia kupanda ulingoni kuzichapa na bondia kutoka malawi Frank Mwamaso katika pambano la raundi nane la uzani wa supermiddle litakalofanyika jijini Dar es salaam.
Nyilawila bondia namba mbili kwa ubora katika uzani wa supermiddle tayari ameisha saini mkataba amesema yupo tayari kupanda ulingoni kwa lengo la kuongeza kiwango cha ubora na mpaka sasa yupo katika mwanzo wa maandalizi kuweza kufanya vizuri katika pambano hilo.
Pambano hilo litasimamiwa na kamisheni ya Ngumi za kulipwa Tanzania( TPBC) chini ya kiongozi wake Chaurembo Palasa.

No comments:

Post a Comment