TANGAZO


Thursday, December 25, 2014

Maadhimisho ya Sikukuu ya Krismasi Dar es Salaam leo

Wanakwaya wa Kanisa la Mtakatifu Albano, wakitumbuiza kwa kwaya wakati wa Ibada ya Misa ya Krismasi kanisani hapo leo. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Waumini wakifuatilia Ibada ya Misa ya Krismasi kwenye Kanisa la Azania Front, Dar es Salaam leo.
Askofu Dk. Alex Malasusa akimsalimia mtoto Mikaella Kamazima (1/8), wakati alipokuwa akiwatakia waumini heri ya Krismasi nje ya kanisa la Azania Front, baada ya kumalizika ibada ya Misa ya Krismasi, Dar es Salaam leo. Kushoto ni baba yake, Michael Kamazima. 
Waumini wa dini ya Kikristo, wakifuatilia ibada ya Misa ya Krismasi katika kanisa la Mtakatifu Albano, Dar es Salaam leo.  
Askofu Dk. Alex Malasusa akiwatakia heri waumini nje ya kanisa la Azania Front, mara baada ya kumalizika ibada ya Misa ya Krismasi, Dar es Salaam leo. 
Waumini wa kanisa la Mtakatifu Joseph, wakitoka nje baada ya kumalizika ibada ya Misa ya Krismasi, iliyokuwa ikiendeshwa na Askofu Msaidizi, Eusebius Nzigilwa, Dar es Salaam leo.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi na familia yake wakiwa kwenye ibada ya Krismasi kwenye kanisa la Mtakatifu Joseph.
Askofu Msaidizi, Eusebius Nzigilwa, akiwaombea waumini wa kanisa la Mtakatifu Joseph, wakati wa ibada ya Misa ya Krismasi, Dar es Salaam leo.
Askofu Msaidizi, Eusebius Nzigilwa, akiwaongoza waumini wa kanisa la Mtakatifu Joseph, kutoka nje mara baada ya ibada ya Misa ya Krismasi, kumalizika kwenye kanisa hilo jijini Dar es Salaam leo.
Wapuliza tarumbeta wa Kanisa la Azania Front, wakipuliza vifaa hivyo wakati waumini walipokuwa wakitoka nje baada ya kumaliza Misa ya Krismasi, Dar es Salaam leo.

No comments:

Post a Comment