TANGAZO


Wednesday, December 10, 2014

Kongamano la Siku mbili la Ukatili wa Kijinsia dhidi ya Wanawake na Walemavu lililoandaliwa na Shirika la Seed Trust lafikia tamati mkoani Morogoro Desemba 9-2014

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Seed Trust, Margareth Mkanga (MB) akizungumza katika kongamano hilo. Kulia ni Mwenyekiti wa Shirika hilo, Stephen Mashishanga. Kongamano hilo la Majadiliano kuhusiana na vitendo vya ukatili kwa wanawake na walemavu limeshirikisha wadau mbalimbali kutoka baadhi ya mikoa ya Tanzania na kuandaliwa na Shirika la Seed Trust la mjini Morogoro kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu Duniani (UNFPA)
Mwenyekiti wa Shirika hilo, Stephen Mashishanga, akichangia mada katika kongamano hilo.
Dk. Ernest Rugiga akitoa mada kuhusu afya ya uzazi.
Mwezeshaji Victor Mulimila akizungumzia kwa ujumla kuhusu vitendo vya ukatili. Kulia ni Dk. Ernest Rugiga.
Ofisa Tarafa wa Manispaa ya Morogoro, Mlange Pakalapakala Jumamosi, akichangia mada kwenye kongamano hilo.
Wanahabari waliokuwepo kwenye kongamano hilo, wakibadilishana mawazo nje ya ukumbi wa Bwalo la JKT, mkoani humo.
Maofisa wa Shirika la Seed Trust wakiwa kwenye kongamano hilo.

Baadhi ya washiriki wa kongamano hilo, wakisikiliza mada zilizokuwa zikiwasilishwa.
Baadhi ya washiriki wakifuatilia mada zilizokuwa zikiwasilishwa kwenye kongamano hilo. (Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com)

No comments:

Post a Comment