TANGAZO


Wednesday, December 31, 2014

“Kampeni ya “Wait to Send” yaendelea Mkoa Dodoma

*Madereva watakiwa kufuata sharia za barabarani
*Abiria watakiwa kutoa taarifa za madereva wazembe

 Ofisa wa Jeshi la Polisi – Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Dodoma, PC Abdala Ramadhani (kushoto) akimpima kiwango cha pombe mwilini dereva wa basi la kwenda mikoani, Keneth Ndahani (katikati) kwa kutumia kifaa maalum wakati wa operesheni ya usalama barabarani iliyofanyika Mkoani Dodoma leo ikiwa ni sehemu ya mwendelezo wa kampeni ya Usalama Barabarani  ya “Wait to Send”  inayohamasisha madereva wa vyombo vya moto kutokutumia simu za mkononi wakati wakiwa wanaendesha vyombo hivyo. Akishuhudia (kulia) ni Meneja wa Vodacom Tanzania Kanda ya Kati Balikulije Mchome.
 Askari wa  Kikosi cha Usalama Barabarani,Mkoa wa Dodoma  PC Athumani Rashid (kushoto) akimpima kiwango cha pombe mwilini dereva wa basi la kwenda mikoani, Haruna Ally(kulia) kwa kutumia kifaa maalum wakati wa operesheni ya usalama barabarani iliyofanyika Mkoani Dodoma  leo ikiwa ni sehemu ya mwendelezo wa kampeni ya Usalama Barabarani  ya “Wait to Send” inayohamasisha madereva wa vyombo vya moto kutokutumia simu za mkononi na kilevi wakati wakiwa wanaendesha vyombo hivyo. Katikati ni Meneja Masoko wa Vodacom Tanzania kanda ya kati Balikulije Mchome.
 Askari wa Kikiosi cha usalama barabarni mkoa wa Dodoma George Daudi (kulia) akimpeleka kituoni cha polisi kondakta wa basi la Shabibya   Alex Chabonga baada ya kumkuta akiendesha gari bila kuwa na leseni jana katika standi kuu ya mabasi mjini Dodoma wakati wa mwendelezo wa kampeni ya Usalama Barabarani  ya “Wait to Send” inayohamasisha madereva wa vyombo vya moto kutokutumia simu za mkononi wakati wakiwa wanaendesha vyombo hivyo pamoja na kuwapima madereva kiwango cha pombe mwilini. Kampeni hiyo imedhamiwa na Vodacom Tanzania.
Mkuu wa Kitengo Cha Elimu wa Jeshi la Polisi – Kikosi cha Usalama Barabarani Tanzania, ACP Abel Swai (kulia)akimpa maelezo dereva wa basi la super Feo Idrisa Abdalah (kushoto) linalofanya safari zake Dodoma -Songea    wakati wa operesheni ya usalama barabarani iliyofanyika Mkoani Dodoma leo kwa kushirikiana na Vodacom Tanzania pamoja na baraza la Taifa la usalama barabarani, ikiwa ni sehemu ya mwendelezo wa kampeni ya Usalama Barabarani  ya “Wait to Send”inayohamasisha madereva wa vyombo vya moto kutokutumia simu za mkononi wakati wakiwa wanaendesha vyombo hivyo pamoja na kuwapima madereva kiwango cha pombe mwilini,Kampeni hiyo inadhamiwa na Vodacom Tanzania.

Mkuu wa Kitengo Cha Elimu wa Jeshi la Polisi – Kikosi cha Usalama Barabarani Tanzania, ACP Abel Swai akisisitiza jambo kwa abiria wa basi la Bunda Expres  wakati wa operesheni ya usalama barabarani iliyofanyika Mkoani Dodoma leo kwa kushirikiana na kampuni ya simu ya Vodacom Tanzania, ikiwa ni sehemu ya mwendelezo wa kampeni ya Usalama Barabarani  ya “Wait to Send”inayohamasisha madereva wa vyombo vya moto kutokutumia simu za mkononi wakati wakiwa wanaendesha vyombo hivyo pamoja na kuwapima madereva kiwango cha pombe mwilini,Kampeni hiyo inadhamiwa na Vodacom Tanzania. 
 Mkuu wa Kitengo Cha Elimu wa Jeshi la Polisi – Kikosi cha Usalama Barabarani Tanzania, ACP Abel Swai akisisitiza jambo kwa abiria wa basi la Bunda Expres  wakati wa operesheni ya usalama barabarani iliyofanyika Mkoani Dodoma leo kwa kushirikiana na kampuni ya simu ya Vodacom Tanzania, ikiwa ni sehemu ya mwendelezo wa kampeni ya Usalama Barabarani  ya “Wait to Send”inayohamasisha madereva wa vyombo vya moto kutokutumia simu za mkononi wakati wakiwa wanaendesha vyombo hivyo pamoja na kuwapima madereva kiwango cha pombe mwilini,Kampeni hiyo inadhamiwa na Vodacom Tanzania.
Mkuu wa Kitengo Cha Elimu wa Jeshi la Polisi – Kikosi cha Usalama Barabarani Tanzania, ACP Abel Swai (kushoto) wakimkabidhi tisheti yenye ujumbe wenye kauli mbiu ya usalama barabarani 2014 dereva  wa basi la Mtei Express Salum Jumanne (katikati) linalofanya safari zake Dodoma na  Arusha wakati wa mwendelezo wa kampeni ya Usalama Barabarani  ya “Wait to Send”inayohamasisha madereva wa vyombo vya moto kutokutumia simu za mkononi wakati wakiwa wanaendesha vyombo hivyo pamoja na kuwapima madereva kiwango cha pombe mwilini anaeshuhudia kulia ni Meneja Masoko wa Vodacom Tanzania kanda ya kati Balikulije Mchome.

Na Mwandishi Wetu, Dodoma
KAMPENI ya usalama barabarani ya kuwataka madereva nchini kuzingatia sheria za usalama barabarani iliyozinduliwa hivi karibuni na Waziri wa Mambo ya Ndani,Mheshimiwa Mathias Chikawe,leo imeendelea katika Mkoa wa Dodoma.
Madereva wameendelea kuhimizwa kutotumia vinywaji vyenye ulevi na kuacha tabia ya kuongea na simu au kutuma na kupokea ujumbe wa maneno (sms) wanapokuwa wanaendesha vyombo vya moto.
Vilevile polisi wa kikosi cha usalama barabarani mkoani Dodoma ambako ni barabara kuu inayotumiwa na magari mengi yaingiayo na yatokayo nchi za jirani walitoa elimu kwa abiria jinsi ya kutoa taarifa waonapo vitendo vya madereva wanaondesha magari kwa uzembe na kuhatarisha maisha yao ambapo walipatiwa namba  maalumu za simu za kutoa taarifa za matukio hayo.
 Kamanda wa elimu usalama barabarani Tanzania ACP Abel Swai amesema kampeni hii ni muhimu katika kupunguza matukio ya ajali “Watumiaji wa barabara hii ya mkoa wa pwani ni wengi hususani madereva wa vyombo vya moto hawana budi kuzingatia maelekezo ambayo tumekuwa tukiwapa katika kampeni hizi ili tupate matokeo mazuri kwa kupunguza ajali kama ilivyokusudiwa”Alisema.

Alisema madereva wakizingatia sheria za barabarani  kwa kiasi kikubwa ajali zinazoendelea kutokea kila siku zitapunga hususani katika kipindi hiki cha msimu wa sikukuu ya  mwaka mpya na aliipongeza kampuni ya Vodacom kwa kuunga mkono jitihada za serikali katika kupambana na tatizo hili ambalo limekuwa sugu.

Kwa upande wake, Kaimu  Masoko wa Vodacom Tanzania kanda ya kati Balikulije Mchome, alisema Vodacom itaendelea  kushirikiana na serikali kuunga mkono jitihada za kuondoa  matatizo kwenye jamii kama lilivyo tatizo hili la ajali ili kuhakikisha wananchi wanaishi maisha murua na marefu.
”Tunatoa rai kwa madereva wote kuzingatia kauli mbiu ya Wiki ya Nenda Kwa Usalama barabarani isemayo”Maamuzi yako barabarani ni hatma yetu-Fikiri kwanza".

 Aliongeza kuwa Vodacom itakuwa mstari wa mbele kuelimisha jamii athari za kuendesha gari wakati huo huo unatumia simu  ya mkononi  kupitia kampeni  ya "Wait to Send" pia itaendelea kuhamasisha madereva kuzingatia sheria za usalama barabarani.
 Alisema kabla ya uzinduzi wa kampeni ya leo tayari umefanyika uhamasishaji wa madereva kuzingatia sheria za barabarani katika miji ya Dar es Salaam,Mwanza,Arusha,Mbeya,Morogoro na kampeni hizi zitaendelea kufanyika sehemu mbalimbali nchini.
Katika kampeni ya leo wafanyakazi wa Vodacom kwa kushirikiana na askari wa  usalama barabarani  na wajumbe wa Baraza la Taifa la Usalama Barabani walitoa uhamasishaji kwa madereva kuacha kuongea na simu wanapoendesha vyombo vya moto na kuwagawia madereva pete maalum za kuwatahadharisha kutotuma ujumbe wa simu za mkononi wanapokuwa wanaendesha vyombo vya moto pia zoezi la kupima madereva kubaini kama wanatumia vilevi lilifanyika ambapo madereva waliokutwa wanaendeshwa vyombo vya moto walichukuliwa hatua kali za kisheria.

Baadhi ya abiria walioshuhudia kampeni hii mkoani Pwani wamesema ni ya muhimu itasaidia kupunguza ajali nchini.
”Hivi sasa ajali nyingi zinazotokea hapa nchini zinasababishwa na uzembe wa madereva,kampeni hizi zikiendelea zitapunguza ajali kwa kiasi kikubwa”.Alisema Muna Abbakari mkazi wa Singida aliyekuwa safarini akitokea Dodoma kwenda Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment