Washiriki wa mafunzo ya ujasiriamali wakifuatilia mafunzo hayo.
Mwelimishaji kutoka Benki ya Posta Tanzania (TPB), akitoa elimu ya ujasiriamali wakati wa semina hiyo.
Washiriki wa mafunzo ya ujasiriamali wakisikiliza elimu ya ujasiriamali iliyokuwa ikitolewa katika semina hiyo.
Washiriki wa mafunzo ya ujasiriamali wakisikiliza elimu ya ujasiriamali iliyokuwa ikitolewa katika semina hiyo.
Washiriki wa mafunzo ya ujasiriamali wakiwa katika semina yao hiyo leo, jijini Mbeya.
Washiriki wa mafunzo ya ujasiriamali wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Maofisa wa Benki ya Posta Tanzania (TPB), wakati wa semina yao jijini Mbeya leo.

Na Mwandishi Wetu
BENKI ya Posta
Tanzania (TPB), kupitia tawi lake la Tunduma, imetoa semina ya mafunzo kwa
wajasiriamali wa Tunduma, Wilaya ya Momba.
Semina hiyo iliyohudhuriwa na
wajasiriamali wapatao mia moja,ililenga kuwaelimisha wafanyabiashara
hao kuhusu matumiza mazuri ya huduma za kibenki,hususan mikopo
inayotolewa na benki hiyo.
Akifungua semina hiyo,
Mkuu wa Wilaya ya Momba Abiudy Saideya, aliipongeza benki ya Posta kwa
kutoa mafunzo hayo ambayo aliamini yatawasaidia wafanyabiashara wa
Tunduma kukuza uelewa wa matumizi sahihi ya huduma zinazotolewa na
taasisi za fedha.
Alisema kuwa wafanyabiashara ni muhimu wakachukua
mikopo ili kukuza mitaji yao na kuongeza uzalishaji,lakini bila kuwa na
elimu sahihi juu ya matumizi ya mikopo hiyo faida yake inaweza
isipatikane.
"Nawashauri wafanyabiashara mnaohudhuria semina hii kutimia
fursa hii kujadiliana ba benki ya Posta ili mfikie muafaka katikati
huduma mnazozitaka".
Pia aliwaasa wafanyabiashara hao kujiepusha na
biashara haramu zitokanazo na bidhaa haramu zilizozagaa mpakani mwa
wilaya yao, kwani kwa kufanya hivyo bishara zao zitataifishwa na hivyo
kupoteza mitaji yao.
Mkurugenzi wa Mikopo
wa benki ya Posta Henry Bwogi iliwasisitiza wafanyabiashara hao
kutembelea tawi la benki hiyo lililopo hapo Tunduma, ili kujipatia
huduma zote za kibenki hususan mikopo itakayowawezesha kukuza mitaji
yao.
Alisema kuwa benki yake inatoa mikopo ya aina nyingi,kuanzia ile ya
vikundi hadi ya wafanyabiashara wakubwa, na riba zinazotozwa na benki
hiyo ni za nafuu sana .
No comments:
Post a Comment