TANGAZO


Saturday, November 1, 2014

Wamisri wakataliwa kuingia Tripoli

Wapiganaji wakilinda uwanja wa ndege wa Tripoli baada ya kuuteka
Mamia ya raia wa Misri wamekataliwa kuingia Libya kwa kupitia uwanja wa ndege wa mji mkuu, Tripoli.
Wafanyakazi katika uwanja wa ndege wa Maitiga waliiambia BBC kuwa wameamrishwa na maafisa wa uhamiaji, wasiruhusu raia wa Misri kuingia Libya hadi amri nyengine itolewe.
Raia kadha wa Misri wamenasa uwanja wa ndege.
Misri imeshutumiwa na makundi ya wapiganaji wanaodhibiti Tripoli kuwa iliwarushia mabomu washirika wa wapiganaji hao katika mji wa pili kwa ukubwa, Benghazi.
Wapiganaji hao walivamia uwanja wa ndege wa Tripoli mwezi Agosti na kuilazimisha serikali ya Libya inayotambuliwa kimataifa kukimbilia Tobruk, mashariki mwa nchi.

No comments:

Post a Comment