TANGAZO

Sunday, November 23, 2014

HPSS Yaiwezesha Dodoma Kuondokana na Tatizo la Uhaba wa Madawa na Vifaa Tiba

Mratibu wa Mradi wa Health Promotion and System Strengthening (HPSS) ambao pia unajulikana kama ‘Tuimarishe Afya Project’ unaofadhiliwa na serikali ya Uswisi,  HPSS, Bi. Fiona Chilunda Akikabidhi,  Compyuta kwa, Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mkoa wa Dodoma, Dk. Ezekiel Mpuya ili kuimarisha upatikanaji wa madawa muhimu na vifaa tiba kwa Mkoa wa Dodoma, kupitia kwa mzabuni mmoja kwa Mkoa wa Dodoma.

Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mkoa wa Dodoma, Dk. Ezekiel Mpuya akipokea shehena ya pili ya dawa na vifaa tiba kwa Mkoa wa Dodoma toka kwa  Meneja Masoko  wa  Bahari Limited, Dk. Tecla Kambanyuma, katika urataribu mpya wa usambazaji dawa kupitia kwa mzabuni mmoja. Wanaoshuhudia ni Mratibu wa HPSS, Fiona Chilunda, wanaoratibu mradi huo. Mradi wa Health Promotion and and System Strengthening (HPSS) ambao pia unajulikana kama ‘Tuimarishe Afya Project  unaofadhiliwa na Serikali ya Uswisili kuimarisha upatikanaji wa dawa muhimu na vifaa tiba kwa Mkoa wa Dodoma, kupitia kwa mzabuni mmoja kwa Mkoa wa Dodoma. Hafla hiyo ilifanyika hivi karibuni mjini Dodoma.

Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mkoa wa Dodoma, Dk. Ezekiel Mpuya akipokea shehena ya pili ya dawa na vifaa tiba kwa Mkoa wa Dodoma toka kwa  Meneja Masoko  wa  Bahari Limited, Dk. Tecla Kambanyuma, katika urataribu mpya wa usambazaji dawa kupitia kwa mzabuni mmoja. Wanaoshuhudia ni Mratibu wa HPSS, Fiona Chilunda, wanaoratibu mradi huo.

Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mkoa wa Dodoma, Dk. Ezekiel Mpuya akizungumza baada ya kupokea shehena hiyo.
Mratibu wa, Mradi wa Health Promotion and System Strengthening (HPSS), ambao pia unajulikana kama ‘Tuimarishe Afya Project’ unaofadhiliwa na serikali ya Uswisi,  HPSS, Bi. Fiona Chilunda, akizungumza baada ya kukabidhi shehena hiyo.

MRADI wa Health Promotion and System Strengthening (HPSS) ambao pia unajulikana kama ‘Tuimarishe Afya Project’ unaofadhiliwa na Serikali ya Uswisi,  umeanza kuleleta neema ya upatikanaji wa dawa muhimu na vifaa tiba kwa Mkoa wa Dodoma, baada ya madawa hayo sasa, kuanza kupatikana kwa wingi na kwa wakati, baada ya kuanza kwa utekelezaji wa madawa hayo kupitia kwa mzabuni mmoja kwa Mkoa wa Dodoma.

Akizungumza wakati wa makabidhiano ya vifaa vua ofisi ya kupokea madawa muhimu na vifaa tiba kutoka kwa Mzabuni mmoja, Mratibu wa HPSS, Tuimarishe Afya, Bi. Fiona Chilunda, amesema,  ili kuhakikisha zoezi la usambazaji wa madawa muhimu linakwenda vizuri, Mradi wa HPSS, unaendelea kuijengea uwezo, bohari ya madawa ya Hospitali Kuu ya Mkoa wa Dodoma, kwa kuipatia vitendea kazi vya kisasa zikiwemo thamani za ofisi, na Comptures za kisasa vilivyogharimu zaidi ya shingi milioni 15 za Kitanzania.

Akizumgumzia mapokezi ya vifaa hivyo, ambavyo vimekwenda sambamba na mapokezi ya shehena ya pili ya madawa kupitia kwa mzabuni mmoja, Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mkoa wa Dodoma, Dk. Ezekiel Mpuya ameishukuru HPSS, kulimaliza tatizo sugu la upatikanaji wa madawa kwa kugharimia mchakato wa upatikanaji wa mzabuni mmoja  kuwasambazia madawa na kuwajengea uwezo wa usambazaji wa madawa muhimu na vifaa tiba, ambapo sasa hospitali yake, wanauhakika wa kuwa na upatikanaji wa madawa wakati wote.

Naye Meneja Masoko  wa Duka la Madawa la Bahari Pharmacy, ambaye ndie aliyeshinda zabuni ya usambazaji wa Madawa kwa Mkoa wa Dodoma, Dk. Tecla Kambanyuma, amewahakikishia kufikisha madawa kwa wakati na sio kusubiri hadi madawa yaishe ndipo walete mengine, bali watakuwa wakileta madawa ya kutosha na kuyahifadhi hapo hapo Dodoma.

Mradi wa HPSS ulizinduliwa mwaka 2011 ukilenga kuusaidia mkoa wa Dodoma kwa kipindi cha miaka Kumi katika sekta ya Bima ya Afya, uboreshaji wa afya ya jamii, usimamiaji wa dawa na usimamiaji wa matengenezo ya vifaa vya afya, mradi huu umefadhiliwa na Ubalozi wa Uswisi nchini Tanzania na unatekelezwa na Shirika la The Swiss Tropical and Public Health Institute (Swiss TPH) likishirikiana na Shirika la Ujerumani la The Micro Insurance Academy (MIA) pamoja na Shirika la The Ifakara Health Institute la Tanzania.

Usambazaji wa madawa kupitia kwa Mzabuni mmoja kwa Mkoa wa Dodoma, kulizinduliwa na Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Mhe. Dkt. Steven Kebwe mwezi September mwaka huu, ambapo alielezea matumaini yake kwa HPSS, ambao wanasimamia mradi wa CHF iliyoboreshwa kwa mafanikio makubwa.

Waziri Kebwe, aliupongeza Mradi huu ambao ni sehemu ya ushirikiano kati ya Serikali ya Uswisi na Tanzania katika kuleta maendeleo na kuboresha afya za wananchi ambao umelenga kukabiliana na upungufu na dawa na vifaa tiba katika Hospitali mbalimbali ili kuboresha afya zawananchi kwa kuwahakikishia upatikanaji wa huduma za tiba zilizobora na za uhakika.

Kiongozi wa kikosikazi cha mradi huo  HPSS kwa hapa nchini, , Profesa Manoris Meshack amesema Kampuni binafsi ya Bahari Limited ndiyo itakayokuwa muuzaji mkuu, hivyo oda za kutoka vituo vyote vya afya vya kila wilaya katika mkoa wa Dodoma zitanunuliwa kutoka kwa muuzaji mmoja.
  
No comments:

Post a Comment