Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein akisalimiana na Viongozi mbali mbali alipofika katika viwanja vya Visitors Inn Hotel Jambiani Wilaya ya Kusini Unguja alipofika leo kuzungumza na Mabalozi na Wenyeviti wa Maskani akiwa katika ziara zake za kuimarisha Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Kusini Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein (kushoto) akitia saini kitabu cha wageni leo alipofika katika ukumbi wa Visitors Inn Hotel Jambiani Unguja kuzungumza na Mabalozi na Wenyeviti wa Maskani akiwa katika ziara zake za kuimarisha Chama katika Mkoa wa Kusini Unguja (kushoto) Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kusini Unguja Abdul-Aziz Hamad Vuai.
Wasoma Utenzi Nezi Khamis na Amina Haji kutoka Jambiani wakihani utenzi wao wakati wa Mkutano wa Mabalozi na Wenyeviti wa Maskani katika ukumbi wa Visitors Inn Hotel Jambiani Wilaya ya Kusini akiwa katika ziara zake za kuimarisha Chama cha Mapinduzi CCM katika Mkoa wa Kusini Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein (katikati) Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai (kulia) Mwenyekiti wa Wilaya ya Kusini Unguja Abdul-Aziz Hamad Vuai wakiwa katika ukumbi wa Visitors Inn Hotel Jambiani Wilaya ya Kusini Unguja katika mkutano maalum wa kuimarisha Chama kwa Mabalozi na Wenyeviti wa Wilaya hiyo.
Mabalozi na Wenyeviti wa Maskani Wilaya ya Kusini Unguja wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein alipookuwa akizungumza na Viongozi hao wa Mashina wa Jimbo la Muyuni katika ukumbi wa Visitors Inn Hotel Jambiani Wilaya Kusini akiwa katika ziara zake za kuimarisha Chama Mkoa wa Kusini Unguja leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein akipokea utenzi kutoka kwa Amina Haji wakati wa mkutano wa Mabalozi na Wenyeviti wa Maskani katika ukumbi wa Visitors Inn Hotel Jambiani Wilaya Kusini akiwa katika ziara zake za kuimarisha Chama cha Mapinduzi CCM katika Mkoa wa Kusini Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein akipokea Risala ya Mabalozi na Wenyeviti wa Maskani katika ukumbi wa Visitors Inn Hotel Jambiani Wilaya Kusini wakati wa Mkutano maalum wa kuimarisha Chama cha Mapinduzi CCM katika Mkoa wa Kusini Unguja.
Mwenyekiti wa Wilaya ya Kusini Unguja Abdul-Aziz Hamad Vuai akionesha Ilani ya Chama kwa Mabalozi na Wenyeviti wa Maskani wakati wa Mkutano maalum wa kuimarisha Chama uliofanywa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk..Ali Mohamed Shein katika Jimbo la Muyuni katika ukumbi wa Visitors Inn Hotel Jambiani Wilaya Kusini.
Balozi wa Shina namba 8 Jimbo la Makunduchi Tawi la Kizimkazi Dimbani Mwajuma Ramadhan Ali akitoa mchango wake mbele ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein wakati alipofika kuzungumza na Mabalozi wa Wilaya ya Kusini Unguja leo katika ukumbi wa Visitors Inn Hotel Jambiani Unguja akiwa katika ziara zake za kuimarisha Chama cha Mapinduzi CCM katika Mkoa wa Kusini Unguja.
Said Ameir, Zanzibar
WANANCHI
wa Zanzibar wametakiwa kutokubali kurubuniwa na watu wanaojidai kutetea maslahi
ya Zanzibar kwa kupinga Katiba iliyopendekezwa na kubainisha kuwa lengo la watu
hao ni kurudisha nyuma maendeleo ya Zanzibar.
Akizungumza
na viongozi wa Mashina na Maskani za Chama cha Mapinduzi wa wilaya ya Kusini
Unguja leo, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali
Mohamed Shein amesema kuwa kitendo cha watu hao kuipinga Katiba iliyopendekezwa
kinamaanisha kudhoofisha jitihada za serikali na wananchi wa Zanzibar za
kujiletea maendeleo.
Dk.
Shein alifafanua kuwa baadhi ya watu hao walikuwa wamesimama kidete kutaka
masuala ya mafuta yashughulikiwe kwa kufuata Sera na Sheria za Zanzibar lakini
leo wamegeuka kupinga jambo hilo kwa kuikataa Katiba ambayo inalitekeleza suala
hilo.
“Watu hawa ni vigeugeu…wakati walishiriki kupitisha
na kuamua azimio la kutaka Zanzibar ichimbe mafuta na gesi kwa kutumia Sera na
Sheria zake badala ya kuwa suala la muungano leo hii jambo hilo limetekelezwa
katika Katiba iliyopendekezwa wanaipinga” Dk. Shein aliwaeleza viongozi hao na
kusisitiza kuwa watu hao wapuuzwe na wala wasipewe nafasi ya kuivuruga Zanzibar.
Alifafanua
kuwa watu hao ni wapinga Muungano na kuwa wanafanya kila hila za kuuvunja na kueleza
kuwa wanafahamu fika kuwa “endapo Katiba iliyopendekezwa itapitishwa itakuwa
imemaliza fitina zao za kutaka kuvunja Muungano” Dk. Shein alieleza.
Alisema
kuwa haiingii akilini kuona watu wanapinga jambo hilo na kuizuia Zanzibar isiweze
kuendelea na jitihada zake za kuendeleza sekta ya mafuta na gesi kwa kizingizio
cha kuipinga Katiba.
“wanataka
Zanzibar tubaki nyuma wakijua kuwa tukiweza kuchimba gesi na mafuta tutaweza
kupiga hatua za haraka. Hivi sasa Tanzania bara wanachimba mafuta na gesi na
majirani zetu wote” Dk. Shein alisema na kusisitiza kuwa nia ya watu hao ni
kuona Zanzibar inabaki nyuma na wao wanapata la kusema.
Kwa
hivyo alitoa wito kwa wananchi wa Zanzibar kuchukua tahadhari na kuisoma kwa
makini Katiba iliyopendekezwa ili waweze kufanya maamuzi sahihi wakati
watakapotakiwa kuipigia kura.
Aliwatahadharisha
wananchi hao kuwa wasisahau kuwa bado wapo watu wanaoitaka Zanzibar kwa kuwa
baadhi yao wanaamini kuwa Mapinduzi yaliwaonea na ndio maana kila wazanzibari
wanaposimama majukwani kutamka Mapinduzi daima wao inawauma na kuchikizwa na kauli
hiyo.
Wakati
huo huo Dk. Shein amewahakikishia wananchi wa wilaya ya Kusini Unguja kuwa
Serikali itaendelea kuimarisha huduma za jamii kwa kuzitafutia ufumbuzi changamoto
mbalimbali zinazokwamisha ufanisi katika utoaji wa huduma bora na kwa wakati
kwa wananchi.
Akijibu
baadhi ya maelezo ya viongozi katika mkutano huo, Dk. Shein alieleza kuwa tatizo
la ukosefu wa madaktari katika hospitali ya mkoa ya Makunduchi, Kivunge na pamoja
na vituo vingine vya afya katika mkoa wa Kusini Unguja amelipokea kwa uzito
unaostahiki na ataiagiza wizara kulishughulikia haraka.
“Lengo
la Serikali ni kuhakikisha kuwa hospitali hiyo ya Makunduchi na Kivunge zinapata
watumishi wa afya wa kutosha wakiwemo madaktari ili huduma zitolewazo ziweze
kwenda sambamba na lengo la Serikali la kuzipandisha hadhi hospitali hizo”.
Kuhusu
suala la Shirika la Umeme-ZECO na Mamlaka ya Maji Zanzibar –ZAWA kuwakatia wateja
wanaochelewesha malipo ya huduma, Dk. Shein aliahidi kuwasiliana tena na
uongozi wa taasisi hizo kuwataka kutoa taarifa mapema kabla zoezi la kukata
huduma kuanza.
Hata
hivyo aliwakumbusha wananchi kuwa taasisi hizo zinayo mamlaka ya kusitisha
huduma kama hawatakuwa wanalipa bili zao hivyo nao wanapaswa kulipa bili zao
kama itakiwavyo.
Mapema
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kusini Bwana Abdulaziz Hamad Ibrahim alipongeza
Serikali kwa kutimiza ahadi zake katika Mkoa huo ikiwemo uimarishaji wa huduma
za afya, maji na uboreshaji wa Halmashauri pamoja na kusifu ufuatiliaji wa utekelezaji
wa ahadi za Rais unaofanywa na wasaidizi wa Mhe Rais.
Kwa
upande wake Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai, alisisitiza
umuhimu wa wananchi kuisoma Katiba iliyopendekezwa ili kupambana na upotoshwaji
wa makusudi wa maudhui ya Katiba hiyo unaofanywa na baadhi ya viongozi wa
upinzani kwa maslahi yao ya kisiasa.
“Katiba
hiyo ina maslahi makubwa kwa pande zote lakini tunaweza kusema kuwa wakati mwingine
wenzetu wa Tanzania Bara wameonesha uungwana sana wa kukubali baadhi ya mambo ambayo
ni dhahiri yameipa maslahi zaidi Zanzibar kuliko Tanzania Bara”







No comments:
Post a Comment