Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein akisalimiana na Viongozi mbali mbali alipofika katika Hoteli ya Bravo Club Kiwengwa Wilaya ya Kaskazini A Unguja kuzungumza na Mabalozi na Wenyeviti wa Maskani katika ziara zake za kuimarisha Chama Mkoa wa Kasakazini Unguja leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein akisalimiana na Viongozi mbali mbali alipofika katika Hoteli ya Bravo Club Kiwengwa Wilaya ya Kaskazini A kuzungumza na Mabalozi na Wenyeviti wa Maskani akiwa katika ziara zake za kuimarisha Chama cha Mapinduzi katika Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein (kulia) akifuatana na Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Meja Mstaafu Juma Kassin Tindwa (kulia) na Mwenyekiti wa CCM Kaskazini Unguja Juma Haji Juma mara alipowasili katika Hoteli ya Bravo Club Wilaya ya Kaskazini A Unguja kuzungumza na Mabalozi na Wenyeviti wa Maskani katika kuimarisha Chama.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein akiingia katika Ukumbi wa Hotel ya Bravo Club Kiwengwa Wilaya ya Kaskazini A Mkoa wa kaskazini Unguja kuzungumza na Mabalozi na Wenyeviti wa Maskani katika ziara za kuimarisha Chama cha Mapinduzi CCM.
Baadhi ya Mabalozi na Wenyeviti wa Maskani katika Wilaya ya Kaskazini A Unguja wakimkaribisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein akizungumza na Viongozi hao katika Ukumbi wa Hotel ya Bravo Club Kiwengwa wilaya ya Kaskazini A Mkoa wa kaskazini Unguja katika ziara za kuimarisha Chama cha Mapinduzi CCM.
Baadhi ya Mabalozi na Wenyeviti wa Maskani katika Wilaya ya Mfenesini Kichama wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein akizungumza na Viongozi hao katika Ukumbi wa Hotel ya Bravo Club Kiwengwa wilaya ya Kaskazini A Mkoa wa kaskazini Unguja katika ziara za kuimarisha Chama cha Mapinduzi CCM.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein (kushoto) akitia saini kitabu cha wageni alipofika katika ukumbi wa Hoteli ya Bravo Club Wilaya ya Kaskazini A Unguja kuzungumza na Mabalozi na Wenyeviti wa Maskani katika kuimarisha Chama (kulia) Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai na (kushoto) Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kaskazini A Ali Makame Khamis.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein akiteta jambo na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai (kulia) wakati wa mkutano wa maalum wa kuimarisha Chama cha Mapinduzi CCM kwa Mabalozi na Wenyeviti wa Maskani Wilaya ya Kaskazini A Mkoa wa Kaskazini Unguja leo.
Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk. Ali
Mohamed Shein (katikati), Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai
(kulia) Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kaskazini A Ali Makame Khamis wakiwa katika ukumbi wa Hoteli ya Bravo Club Wilaya ya Kaskazini A
Unguja kuzungumza na Mabalozi na Wenyeviti wa Maskani katika kuimarisha Chama.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein
akizungumza na Mabalozi na Wenyeviti wa Maskani
katika ukumbi wa Hotel ya Bravo Club Kiwengwa wilaya ya Kaskazini A Mkoa
wa kaskazini Unguja katika ziara za
kuimarisha Chama cha Mapinduzi CCM.
Na Rajab Mkasaba, Ikulu
Zanzibar
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar
Dk. Ali Mohamed Shein amesema kuwa CCM itaendelea kuyalinda Mapinduzi matukufu
ya Januari 12, 1964 pamoja na Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kwa maslahi ya
wananchi wote wa Tanzania.
Hayo aliyasema leo, katika Mkutano kati yake na viongozi wa Mashina na
Maskani za CCM Wilaya ya Kaskazini A Unguja, Mkutano uliofanyika katika ukumbi
wa Hoteli ya ya Bravo Kiwengwa, Wilaya ya Kaskazini A Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Katika hotuba yake kwa viongozi hao Dk. Shein alisema kuwa kuna kila sababu
ya kuyaendeleza na kuyalinda Mapinduzi pamoja na Muungano uliopo kama
zilivyofanya awamu zote zilizopita kwani hizo ndio ngao za nchi hii.
Alisisitiza kuwa hakuna mabadala wa Muungano wala Mapinduzi ya Januari
12,1964 na kuwataka viongozi hao kuhakikisha wanazilinda ngao hizo kwa maslahi
ya wananchi wote wa Tanzania.
Aidha, Dk. Shein aliwashangaa wale wote wanaotaka kurejesha Katiba ya mwaka
1963 ambayo ni katiba ya Mkoloni na ambayo ilikuwepo kwa maslahi ya Sultani na
si kwa Wazanzibari ambao ndio waliokuwa wenye nchi.
Sambamba na hayo, Dk. Shein aliwataka wanaCCM pamoja na Mashekhe wa Mkoa
huo kujibu hoja kwa ustarabu hasa zile zinazoletwa kwa visingizio vya kidini
huku zikichanganywa na siasa na kusisitiza kuwa si jambo la busara kugombanisha
watu kwa kisingizio cha dini.
Alisisitiza kuwa siasa na dini ni vitu viwili tofauti wala siasa sio vurugu
na kuwasifu wanaCCM wa Kaskazini kwa juhudi zao hasa kwa historia yao ya
ukombozi wa Zanzibar na ndio maana wamekuwa hawatetereki.
Dk. Shein pia, aliwaeleza viongozi hao kuwa chama hicho kinawajali na
kinawathamini smbamba na kutambua juhudi zao na kuwahakikishia kuwa kitaendelea
kuwanga mkono na kushirikiana nao kwa kutambua umuhimu wao huku akiwaeleza jukumu
la CCM ni kuimarisha amani na utulivu nchini.
Katika suala zima la ujenzi wa miundombinu ya barabara Dk. Shein alieleza
kuwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imefanya juhudi ya kuagiza vifaa vya ujenzi
wa barabara ili kutatua tatizo la miundombinu hiyo kwani tatizo kubwa hivi sasa
ni kuwepo kwa uhaba wa vifaa hivyo hapa nchini.
Aidha, Dk. Shein alieleza kuwa tatizo la maji katika eneo la Kijini
litatafutiwa ufumbuzi wa haraka pamoja na maeneo mengine sambamba na kutafutiwa
ufumbuzi changamoto nyengine zinazowakabili wananchi wa maeneo hayo.
Nae Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai alieleza kuwa
wapinzani hawataki Muungano wa aina yeyote na wamekuwa wakitoa visingizio
visivyo na msingi na hivi sasa wameamua kuunga mkono Katiba ya Mkoloni ya mwaka
1963 ambayo hivi karibuni katika kongamano lao waliisifu kwa kudai itawasaidia
Wazanzibari.
Vuai alisema mtu mwenye akili hawezi kuisifu Katiba ya mwaka 1963 kwani
katika hiyo katika kifungu cha 3, inamtambua Sultani kuwa ndie Mkuu wa nchi na
Mawaziri wote anawachagua yeye kuendesha Serikali, na kwa mujibu wa Katiba hiyo
atarithiwa na vizazi hatua ambayo ndio iliyowafanya wazee wakati huo kufanya
Mapinduzi.
Naibu Katibu Mkuu huyo alisema kuwa kama kuna mambo ambayo Wazanzibari
wanafaidika nayo ni pamoja fursa iliyopo katika elimu ya juu kupitia Bodi ya
mikopo ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na ile ya Zanzibar na kueleza
kuwa jambo hilo limo kwenye Katiba inayopendekezwa kwani Wazanzibari wamekuwa
wakipata fursa zote mbili za kupata mikopo hiyo.
“Kati ya mwaka 2012 na 2013 vijana wa Kizanzibari wapatao 860 walipata mkopo katika Bodi ya Mikopo ya
Zanzibar ba kwa upande wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu ya Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania vijana 1024 wa Kizanzibari walipata mkopo, je hapo utasema Muungano
hauna faida.. hakuna sababu kwa vijana hasa wasomi kutoiunga mkono Katiba
inayopendekezwa”alisema Vuai.
Aidha, viongozi hao wa Wilaya ya Kaskazini A walitoa pongezi kwa Dk. Shein
kwa kusimamia amani na usalama hasa pale kulipojitokeza kikundi cha dini na kujiingiza
kwenye siasa kikiwa na azma ya kutaka kuvuruga amani iliyopo nchini.
Katika risala yao viongozi hao walieleza furaha yao waliyonayo kutokana na juhudi za Dk. Shein katika utekelezaji wa Ilani
ya uchaguzi wa CCM ya mwaka 2010-2015 katika maendeleo kwenye sekta mbali mbali
ikiwa ni pamoja na kukamilika kwa skuli za Sekondari za Matemwe na Chaani
ambazo tayari zimekamilika na hivi sasa zinatoa huduma.
Viongozi hao walieleza kuwa Hospitali ya Kivunge imepanuliwa na huduma nyingi
sasa zinatolewa na na kituo cha afya
kilichopo Pwanimchangani tayari kimeshafunguliwa na kusisitiza kuwa mradi
mkubwa wa usambazaji maji kwenda Nungwi kupitia Matemwe na Kijini unaendelea
vizuri na hivi karibuni mradi huo unatarajiwa kukamilika.
Aidha, kupitia kwa Dk. Shein viongozi hao walitoa shukurani za dhati kwa Mama
Mwanamwema Shein kwa kushirikiana na Mama Asha Suleiman Idd na baadhi ya wake
wa Wabunge na Wawakilishi wa CCM kwa kuanzisha na kuendeleza Umoja wao wenye
azma ya kuimarisha Chama sambamba na kuwaendeleza akina mama katika vikundi vya
uzalishaji mali pamoja na madrasa.
Pamoja na hayo, viongozi hao walieleza haja ya kufanywa taratibu ili somo
la historia lisomeshwe kuanzia skuli za msingi
kwani vijana walio wengi hawaifahamu
historia ya nchi yao jambo ambalo
linawaburuza vijana kushawishiwa kirahisi na kujiingiza katika makundi
yasiokuwa na faida.

No comments:
Post a Comment