TANGAZO


Saturday, October 4, 2014

Michezo shimiwi: Kilimo yaibanjua Sheria 5-4, Mambo ya Ndani yaipiga Ardhi 1-0 mjini Morogoro

Beki namba 5 wa timu ya soka ya Ardhi, Selemani Kungulilo (kushoto) akiwania mpira pamoja na beki  wa timu ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Seif Kibangu (kulia) katika mchezo wa SHIMIWI uliofanyika leo uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro. Mambo ya Ndani ilishinda kwa bao 1-0.(Picha zote  na Happiness Shayo)
Timu ya soka ya Mambo ya Ndani ya Nchi baada ya mechi kati yake na Ardhi katika Uwanja wa Jamhuri, mjini Morogoro leo.
Timu ya soka ya Kilimo kabla ya mpambano dhidi yake na timu ya Sheria katika Uwanja wa Tumbaku, mjini Morogoro. Kilimo ilifunga mabao 5-4.
Timu ya soka ya Sheria kabla ya kuanza kwa mpambano dhidi yake na Kilimo uliofanyika uwanja wa Tumbaku mjini Morogoro. 
Wachezaji wa kiungo wa timu ya soka ya Sheria (jezi ya orange), wakimzonga mlinzi wa timu ya soka ya Kilimo, John Tamba katika mchezo wa SHIMIWI uliofanyika Uwanja wa Tumbaku, mjini Morogoro leo.
Mlinda mlango wa timu ya soka ya Sheria Alfani Botea (aliyelala), akipewa huduma ya kwanza baada ya kuanguka uwanjani katika mchezo dhidi ya timu yake na timu ya Kilimo iliyofanyika Uwanja wa Tumbaku, mjini Morogoro leo.

No comments:

Post a Comment