Bi
Tawale alisema kuwa tathmini kuhusu uzingatiaji wa sheria, kanuni na taratibu
za masuala ya ajira iliyofanywa na Tume
hiyo mwaka 2010/2011 katika Wizara, Idara zinazojitegemea, Mamlaka za Serikali
za Mitaa na Sekretarieti za Mikoa imebainisha kuwa kiwango cha uzingatiaji
kimeongezeka hadi kufikia asilimia 64 kwenye vipengele vya Uajiri, Upimaji wa Utendaji Kazi wa Wazi
(OPRAS), Likizo ya Mwaka na Likizo ya Ugonjwa.
Akifafanua
zaidi Bi Tawale aliongeza kuwa ukilinganisha na utafiti wa kwanza uliofanyika
mwaka 2005/2006 ambapo kiwango kilikuwa ni asilimia 50 ongezeko hilo limetokana
na elimu inayotolewa na Tume kwa wadau kuhusu utekelezaji wa Sheria ya Utumishi
wa Umma Na.8 ya mwaka 2002 na Marekebisho yake Na.18 ya mwaka 2007.
“Tume
ya Utumishi wa Umma inajitahidi kuweka mikakati ili kuhakikisha inakabiliana na
changamoto za masuala ya ajira katika kuongeza uzingatiaji wa Sheria, Kanuni na
Taratibu kwa kuendelea kutoa elimu kupitia miongozo, vipindi kwenye vyombo vya
habari na maonyesho mbalimbali ya kitaifa”. Alisema Bi Tawale.
Aidha
Bi Tawale alisema kuwa Mwongozo uliotolewa na Tume hiyo kuhusu masuala ya ajira
katika Utumishi wa Umma unawawezesha Waajiri na Mamlaka za Ajira kufuata
taratibu wanaposhughulikia masuala ya ajira kwenye mamlaka zao.
Aliongeza
kuwa katika kuhakikisha sheria, kanuni na taratibu za ajira zinatekelezwa
ipasavyo Tume huagiza Waajiri au Mamlaka za Ajira kuchukuliwa hatua ikiwemo
kuwaita mbele ya Tume kujieleza ikithibitika wamekiuka sheria au wameshindwa
kutekeleza majukumu yao.
No comments:
Post a Comment