Bi.
Gloria alisema kuwa kiasi hicho cha madawa kimepatikana baada ya uchunguzi wa
majalada 208 yaliyopokelewa na kufanyiwa uchunguzi katika mwaka huo.
“Wakala
wa Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali umefanya Uchunguzi wa vielelezo
vidhaniwavyo kuwa ni dawa za kulevya ambapo majalada 208 yaliyopokelewa kwa mwaka
2013 na kubaini jumla ya kilogram 6,428.12 za dawa hizo”Alsema Bi. Gloria.
Akitaja
idadi ya majalada na sampuli za dawa hizo Bi Gloria alisema kuwa dawa aina ya
Bangi imeongoza kwa kuwa na kiasi kikubwa cha uzito wa sampuli ikiwa na
kilogram 3765.12 kwa idadi ya majalada 72 wakati Heroin imeongoza kwa kuwa na
idadi kubwa ya majalada ambapo majalada 112 yalichunguzwa na kilogram 46.67
ziligunduliwa.
Aina
nyingine ya dawa zilizotajwa ni Cocaine ikiwa na idadi ya majalada mawili
yaliyochunguzwa na kilogram 4.22 ziligunduliwa, majalada 21 ya mirungi yalichunguzwa
na kupatikana kilogram 2579.8 na jalada moja la Ephedrine lilikuwa na kilogram
32.31.
Bi
Gloria aliongeza kuwa shughuli za uchunguzi wa sampuli za dawa hizo umesaidia
utoaji wa ushahidi mahakamani pamoja na kupambana na usafirishaji wa dawa za kulevya.
No comments:
Post a Comment