Fatma
Salum-Maelezo
SERIKALI imejipanga kutatua tatizo la makazi kwa
watumishi wa umma kwa kujenga nyumba Elfu 10 za gharama nafuu kote nchini.
Hayo yamesemwa jijini Dar es Salaam na Mtendaji Mkuu
wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) Bw.Elius
Mwakalinga wakati wa ziara ya waandishi wa habari katika miradi mbalimbali
inayotekelezwa na wakala huo jijini Dar es Salaam na Pwani.
Mwakalinga
alisema kuwa mradi huo wa nyumba elfu 10
unaogharimu zaidi ya shilingi bilioni 18 unahusisha nyumba za viongozi na watumishi
wa kawaida wa kada zote.
“Lengo la
kujenga nyumba hizi ni kuwapatia watumishi wa umma makazi bora jirani na maeneo
yao ya kazi ili kuongeza tija katika utoaji huduma kwa wananchi. Mradi huu
utawawezesha kupata nyumba za kupanga na kununua kwa gharama nafuu”. Alisema Mwakalinga.
Akifafanua zaidi
Mwakalinga alisema kuwa fedha za
kutekeleza mradi huo zinatokana na ruzuku ya serikali pamoja na fedha za TBA
ambapo kwa mkoa wa Dar es Salaam nyumba hizo zimeanza kujengwa kwenye maeneo ya
Bunju, Mbezi Beach, Ada Estate na Masaki na pia eneo la Chalinze mkoani Pwani.
Pia Nnunduma
alisema mpaka sasa ujenzi unaendelea vizuri kwenye mikoa mbalimbali nchini
ikiwemo mikoa mipya ya Katavi, Geita, Simiyu na Njombe.
Naye Meneja wa
Kikosi cha Ujenzi cha TBA Mhandisi Wilfred Dungamu alieleza kuwa kwa sasa wakala
huo unatumia kikosi cha wahandisi wa ndani kilichoanzishwa mwaka 2012 na mpango
huo umesaidia kupunguza gharama kubwa zilizokuwa zikitumika kuwalipa wahandisi
kutoka makampuni binafsi.
No comments:
Post a Comment