Thursday, September 25, 2014
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akishiriki kupanga mawe kwenye msingi wa Kituo cha Afya cha Kijiji cha Kwediboma, wakati wa ziara yake wilayani Kilindi leo.
Kinana akibeba ndoo zenye zege, aliposhiriki katika ujenzi wa jengo la maabara katika Kijiji cha Kibarashi, wilayani Kilindi, Tanga.
Wananchi wa Kijiji cha Kibarashi wakishangilia wakati Kinana alipokuwa akihutubia katika mkutano wa hadhara.
Kinana akisalimiana na Kamanda wa Polisi, Wilaya ya Kilindi, Cleophas Magesa alipowasili wilayani humo.
Wananchi wakiwa wamejipanga kusalimiana na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana katika Kijiji cha Kwediboma ambapo alishiriki katika ujenzi wa jengo la Kituo cha Afya. (Picha aote na Kamanda Richard Mwaikenda wa Kamanda wa Matuko blog)
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akihutubia katika mkutano katika Kijiji cha Kwediboma, wilayani Kilindi.
Kinana akihutubia katika kijiji hicho, ambapo alihimiza wananchi kujenga tabia ya kuchangia shughuli za maendeleo.
Wananchi wa Kijiji cha Kwediboma wakishiriki kubeba mawe kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa msingi wa jengo la kituo cha afya .
Kinana akisalimiana na wananchi wa Kibarashi alipowasili kushiriki ujenzi wa jengo la maabara katika Shule ya Sekondari ya Kibarashi wilayani Kilindi.
Kinana na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga, Henry Shekifu wakisaidiana na mafundi kuchanganya zege kwa ajili ya ujenzi wa maabara ya Shule ya Sekondari Kibarashi, wilayani Kilindi jana.
Wananchi wa Kibarashi wakisalimiana na Kinana alipowasili kwenye mkutano wa hadhara mjini Kibarashi leo.
Wananchi wa Kibarashi wakishangilia baada ya kukunwa na hotuba ya Kinana.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akihutubia katika mkutano wa hdhara katika Kijiji cha Kibarashi.
Kinana akihutubia katika mkutano wa hdhara katika Kijiji cha Kibarashi leo.
Wananchi wakisikiliza kwa makini wakati Kinana akihutubia katika mkutano wa hdhara katika Kijiji cha Kibarashi.
Mmoja wa wanakijiji wa Kibarashi, akiuliza swali kwa Kinana kuhusu matatizo ya huduma za afya kwa wanawake na watoto kijijini hapo.
Kinana akimkabidhi kadi mmoja wa wanachama wapya wa CCM katika mkutano huo.
Baadhi ya wananchama wapya wa CCM, wakila kiapo baada ya kukabidhiwa kadi mpya.
Kinana akiwaongoza wanachama wapya na wa zamani wa CCM kula kiapo katika mkutamo huo.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akihutubia katika mkutano uliofanyika Mjini Songe, Kilindi ambapo aliwataka viongozi kufanya mikutano na wananchi ili kuwaelezea mambo mbalimbali yanayotekelezwa pamoja na kutatua matatizo yao badala ya kusubiri yatatuliwe na viongozi wa juu wanaofanya ziara katika maeneo yao.
Kinana akihutubia katika mkutano wa hadhara mjini Kilindi leo, ambapo aliwataka wananchi kutowachagua viongozi wazembe, walaghai na wasio na kazi.
Sehemu ya umati wa wananchi ukumsikiliza Kinana wakati akihutubia mjini Kilindi leo.
Mkazi wa Kilindi mwenye ulemavua akielezea jinsi anavyoteseka kukosa baiskeli ya kumsadia kurahisisha kazi zake. Kinana baada ya kusikia kilio chake alimsaidia fedha za kununulia baiskeli.
Baadhi ya wanachama w pya wa CCM wakila kiapo katika mkutano huo
Kinana akishiriki ujenzi wa jengo la CCM wilaya ya Kilindi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment