Katibu wa Bunge Maalum la Katiba Yahya Khamis Hamad akiongea
na waandishi wa Habari kuhusu uwasilishwaji wa Sura zilizosalia za Rasimu ya
Katiba Mpya utakaofanywa na Kamati zote 12 za Bunge. Kulia Mkurugenzi wa Idara
ya Habari na Itifaki wa Bunge hilo, Bw.
Jossey Mwasyuka. Mkutano huo ulifanyika 01 Septemba, 2014 kwenye Ukumbi
wa Spika mjini Dodoma.

Baadhi ya Waaandishi wa Habari wakifuatilia kwa makini
taarifa ikiyotolewa na Katibu wa Bunge Maalum la Katiba wakati wa mkutano huo
ulifanyika 01 Septemba, 2014 kwenye Ukumbi wa Spika mjini Dodoma.
Baadhi ya Waaandishi wa Habari wakifuatilia kwa makini
taarifa ikiyotolewa na Katibu wa Bunge Maalum la Katiba wakati wa mkutano huo
ulifanyika 01 Septemba, 2014 kwenye Ukumbi wa Spika mjini Dodoma. (Picha zote na Benedict
Liwenga, Maelezo-Dodoma)
Na Benedict Liwenga, Maelezo-Dodoma.
01/09/2014.
KAMATI 12 za Bunge Maalum la Katiba kesho zitaanza kuwasilisha
Sura zilizosalia za Rasimu ya Katiba Mpya ambazo ni Sura ya Pili, Tatu, Nne na ya
Tano kwa mujibu wa ratiba iliyopangwa tangu tarehe 5 Agosti, Mwaka huu.
Hayo yamesemwa leo na Katibu wa Bunge Maalum la Katiba Yahya
Khamis Hamad wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa Habri kwenye Ukumbi
wa Spika mjini Dodoma.
“Kila Kamati imeshandaa taarifa kwa ajili ya kuiwasilisha katika
Bunge hapo kesho”, alisema Katibu huyo.
Aidha, Katibu huyo ameongeza kuwa baada ya sura hizo
kumalizika, Sura zitakazofuata ni Sura ya Saba, Nane na 14 na nyingine ni sura
mpya.
Ameongeza zaidi kuwa, utaratibu huo utaendelea mpaka sura
zote zitakapomalizika siku ya tarehe 8 Septemba, 2014 saa mbili usiku.
Katibu ameongeza kuwa Bunge hilo litaanza kujadili Sura hizo za
Rasimu ya Katiba Mpya kuanzia siku ya tarehe 9 Septemba, 2014.

No comments:
Post a Comment