TANGAZO


Tuesday, August 5, 2014

Winnie Mandela adai mali ya Hayati

Winnie Mandela anataka nyumba ya marehemu Mandela ikabidhiwe wanawe

Mke wa zamani wa hayati Nelson Mandela, anataka watoto wake wapewe nyumba ya marehemu iliyoko kijijini Qunu.
Hatua hiyo huenda ikazua mgogoro wa kwanza wa kisheria kuhusiana na mali ya hayati Mandela tangu kuaga dunia mwaka jana.
Mali ya hayati Mandela ilikadiriwa kuwa yenye thamani ya dola milioni 4.3 baada ya kifo chake mwezi Disemba mwaka jana.Mawakili wa Winnie Madikizela-Mandela wamesema kudai nyumba hiyo ni haki yake ya kitamaduni kwani aliwahi kuwa mke wa hayati Mandela.
Mzee Mandela alimpa talaka bi Madikizela-Mandela mwaka 1996.
Wawili hao walifanikiwa kupata watoto wawili, Zinzi na Zenani.
Hayati Mandela ana mtoto mmoja kwa jina Makaziwe kutoka kwa ndoa yake ya kwanza kwa marehemu Evelyn Mase.
Wakati wa kifo chake alikuwa amemuoa,Graca Machel, mkewe marehemu Samora Machel, aliyekuwa Rais wa kwanza wa Msumbiji.
'Mila na Tamaduni'
Katika wasia wake, marehemu Mandela alisema: ''Mali yake ya Qunu ikiwemo nyumba hiyo inapaswa kutumiwa na familia yake nzima ili kukuza umoja katika familia hiyo ''
Katika barua hiyo ambayo BBC imeweza kuiona, mawakili walisema kuwa Bi Madikizela-Mandela ndiye alipata nyumba hiyo katika eneo la Qunu, wakati Mandela alipokuwa generezani akipigana dhidi ya utawala wa mzungu.
''Msimamo wetu ni kwamba nyumba hiyo ni mali ya kizazi cha Mandela na Winnie Madikizela-Mandela,'' ilisema barua hiyo.
''Ni katika nyumba hii pekee ambapo watoto na wajukuu wa Madikizela-Mandela wanaweza kuendesha shughuli zao, na nyumba hiyo haiwezi kukabidhiwa kwa mtu yeyote ambaye sio mtoto wala mjukuu wake. ''
Barua hiyo ilisema kuwa haimaanishi kwamba watoto wengine wa Mandela watanyimwa ruhusa ya kuingia katika nyumba hiyo.
"lakini udhibiti na usimamizi wa nyumba unapaswa kufafanuliwa kwa misingi ya kitamaduni na mila,'' walisema mawakili hao.
Simanzi ilitanda kote duniani kufuatia kifo cha Mandela mwaka jana akiwa na umri wa miaka 95.
Alisifika kwa kupigana dhidi ya utawala wa wuzungu na kwa rais wa kwanza mzalendo wa Afrika Kusini baada ya kutoka jela ambako alifungwa kwa miaka 27.

No comments:

Post a Comment