Waziri Mkuu wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mizengo Pinda, akihutubia wakati akifunga
Kongamano la 25 la Wajiolojia Barani Afrika lililofanyika tarehe 14-16 Jijini
Dar es Salaam. Wakati akifunga Kongamano hilo, Waziri Pinda amewataka watafiti
barani Afrika kufanya tafiti ambazo zina mahusiano ya moja kwa moja na jamii
ili tafiti hizo zitumike katika kuwazesha wananchi kufaidika na rasilimali
zilizopo barani Afrika.
Baadhi ya Wajilojia
kutoka nchi mbalimbali barani Afrika wanaohudhuria Kongamano la 25 la
Wajiolojia Afrika wakifuatilia hotuba ya kufungamano hiyo iliyosomwa na Waziri
Mkuu Mizengo Pinda (hayupo pichani).
Waziri Mkuu Mizengo
Pinda katika picha ya pamoja na baadhi ya Wajiolojia waliohudhuria kongamano
hilo kutoka nchi mbalimbali Barani Afrika. Wengine katika picha kutoka kushoto
ni Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ,Sadik Meck
Sadik na Rais wa Wajolojia Afrika Profesa
Aberra Mogassie.
Na Asteria Muhozya, Dar es Salaam
Wajiolojia barani
Afrika wametakiwa kufanya tafiti zenye uhusiano wa moja kwa moja na jamii na
kuzionesha tafiti hizo ili ziweze kutumiwa
kama ufumbuzi wa matatizo
mbalimbali yanayolikabili bara la hilo, jambo ambalo litaiwezesha Afrika
kunufaika na rasilimali zilizopo
na hivyo kuchangia katika ukuaji wa uchumi, maendeleo ya watu na mapato ya
mataifa yao.
“Najua watafiti
wanaweza kusema serikali zetu hazitumii tafiti zetu, lakini mkifanya tafiti
zenye uhusiano wa moja kwa moja na jamii, mkazitoa kwa jamii tutazitumia
msizifungie makabatini,” amesisitiza Pinda.
Hayo yamebainishwa na
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mizengo Pinda leo jijini Dar
es Salaam wakati akifunga kongamano la 25 la Wajiolojia barani Afrika na kueleza kuwa, ili Afrika iweze kuendelea na kufaidika na rasilimali
zake, inahitaji kuzalisha wataalamu wengi
katika taaluma ya sayansi ikiwemo wajiolojia.
“Hapa nchini Tanzania
Profesa Muhongo anapambana sana na taaluma hii, jambo hili litasaidia kuzalisha
wataalamu wengi katika sekta za mafuta na gesi. Lakini na ninyi, mnahitaji
kuzalisha wataalamu ili tuisogeze mbele Afrika,” alibainisha Pinda.
Ameongeza kuwa,
serikali ya Tanzania tayari inajipanga katika kuhakikisha inazalisha watalaam
wengi wa sayansi kupitia programu za Vyuo Vikuu ambapo tayari imeanzisha masomo
ya mafuta na gesi katika baadhi ya vyuo vikuu nchini, hususani Chuo Kikuu cha
Dar es Salaam (UDSM) na Chuo Kikuu Dodoma (UDOM), ikiwemo kampeni ya
kuhakikisha kwamba kila shule ya sekondari inakuwa na maabara ambazo
zitachochea kizazi cha wanasayansi.
Vilevile, amezungumzia tatizo
la Afrika kutokufaidika na rasilimali
zake zilizoko ardhini na kuongeza kuwa,
linatokana na matumizi kidogo ya sayansi yanayofanywa na nchi nyingi za Afrika, hivyo,
amewataka wataalamu hao kuhakikisha wanatoka na njia ambazo zitasaidia
na kuliwezesha bara hilo kuitumia sayansi kwa maendeleo ya nchi zao kwa sasa na
kwa kizazi kijacho.
Aidha, amewataka
wataalamu hao kutumia kuitumia taaluma hiyo zaidi ya inavyotumika sasa ikiwemo
kuhakikisha kwamba afrika inasimama imara kupitia rasilimali zilizopo na
kuiondoa katika matatizo ya kiuchumi, kiafya na kimazingira.
Halikadhalika, amewataka
wataalamu hao, kufikiria namna ambavyo nchi za afrika zitasimamia suala la
uthaminishaji madini katika nchi zao kwa kuhakikisha kwamba, shughuli za
uthamini madini zinafanywa ndani ya Afrika tofauti na sasa ambapo nchi nyngi
bado zinasafirisha madini nje bila kuyathamini
jambo ambalo linachangia katika kuzikosesha nchi hizo mapato stahiki
yanayotokana na rasilimali hiyo.
Kwa upande wake,
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter
Muhongo akizungumza katika mkutano huo, amewataka wajilojia Afrika kufanya
tafiti nyingi za kutosha ili kujua kiasi cha mafuta na gesi ambacho bado kipo Afrika lakini bado hakifahamiki ili
rasilimali hizo zisaidie kubadilisha taswira
ya afrika.
Ameongeza kuwa, Afrika
inatakiwa kujikita zaidi katika kuzalisha wataalamu wa kutosha na kujua namna
ya kuziendelea rasilimali hizo wakati huo huo ikihakikisha kwamba, zinchangia
kwa kiasi kikubwa katika kuinua uchumi, kuvutia uwezaji na kuchangia katika
maendeleo ya watu.
Ameongeza kuwa, bado
afrika inazalisha kiasi kidogo cha nishati ya umeme wakati dunia inahitaji
nishati hiyo kwa kiasi kikubwa hivyo, amewataka wataalamu hao kuhakikisha
wanasaidia katika kuwezesha upatikanaji wa rasilimali hiyo kupitia taaluma zao.
Vilevile, amewataka
wajiolojia afrika kuipa kipaumbele miradi ya umeme vijijini katika nchi zao, na
kuhakikisha kwamba, miradi hiyo kama ilivyo miradi ya REA nchini, inafanyika na
kufanikiwa kwa kiasi kikubwa ikiwemo kufanya tafiti kuhusu miradi hiyo.
Katika hatua nyingine,
Profesa Muhongo amekitaka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Chuo Kikuu Dodoma
kulifanyia kazi suala la ukosefu wa wahadhiri katika vyuo hivyo katika fani za mafuta na gesi na wizara
imehaidi kuhakikisha kwamba inawezesha upatikanaji wa wakufunzi katika masomo
hayo kutoka sehemu mbalimbali duniani.
Naye Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Profesa Nelson Boniface, ameeleza kuwa, kongamnao hilo la siku tatu la
wajiolojia barani Afrika limewawezesha washiriki kujadili masuala mbalimbali
yanayoihusu taaluma hiyo yakiwemo kyanayohusu nishati mchanganyiko, namna ya namna jilojia
inavyoweza kusaidia matatizo ya umaskini, maji, afya na mengineyo yalijadiliwa
katika kongamano hio.
Profesa Boniface ameongeza
kuwa, washiriki wa kongamano hilo walijadili na kuona kwamba, uwepo wa wataalamu waliobobea katika taaluma hiyo ni jambo la msingi kutokana na nafasi na mchango
wao katika kuendeleza , namna ya kutumia
Afrika na dunia zinavyoweza kufaidika na rasilimali hizo.
Akielezea kuhusu
mkutano wa Tatu wa Wanasayansi Vijana Duniani ambao ulitangulia kabla ya kongamano hilo,
ameleza kuwa, mkutano huo uliweza kuwapa
nafasi vijana kujadili masuala mbalimbali kuhusu namna jiolojia inavyoweza
kuchangia kuondoa umaskini na kuwezesha maisha bora kwa jamii ya Afrika
inavyoweza kunufaika na rasilimali asilia na masuala mengine muhimu.
Kongamano la 25 la
Wajilojjia Afrika limewakutanisha wajiolojia waliobobea katika taaluma hiyo kutoka nchi
zaidi ya 42 Afrika na duniani . Aidha, Serikali kupitia Wizara ya Nishati na Madini
imewezesha kufanyika kwa kongamano la wajilojia uliokuwa ufanyike nchini
Brazil.
Aidha, mikutano yote miwili
imedhaminiwa na taasisi na makampuni mbalimbali, ambapo pia kampuni inayofanya
utafiti na uchimbaji wa gesi na mafuta ya BG-Tanzania ilikuwa ndio mdhamini
mkuu wa kongamano hilo.
Kongamano lingine la
Wajiolojia Afrika linatarajiwa kufanyika nchini Afrika kusini.
No comments:
Post a Comment