*Wakabidhiwa zawadi zao
Baadhi ya wadau wa Soko la Hisa la Dar es Salaam DSE pamoja na wanafunzi walioshiriki katika Shindano la Uwekezaji “DSE Scholar Investment Challenge” wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi katika hafla hiyo (hayupo pichani) wakati wa hafla ya kukabidhi zawadi kwa washindi wa shindano hilo leo jijini Dar es Salaam.
Majaji wa shindano la Uwekezaji “DSE Scholar Investment Challenge” wakifuatilia jinsi washiriki (hawapo pichani)wanavyoelezea namna walivyoshawishika kushiriki katika shindano hilo, wakati wa hafla ya kukabidhi zawadi kwa washindi wa shindano hilo iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Mwakilishi wa NMB Benki Bw.George Kivaria akikabidhi Cheti
Ckwa Bi. Anna Chimn mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino (SAUT)
ikiwa ni kutambua ushiriki wake katika shindano la Uwekezaji “DSE Scholar Investment Challenge” wakati wa
hafla ya kukabidhi zawadi kwa washindi wa shindano hilo leo jijini Dar es
Salaam.Jumla ya wanafunzi 50 kati ya wanafunzi 5000 waliojitokeza kushiriki
katika shindano hilo walekabidhiwa vyeti vya ushiriki.
Mkuu wa Mtandao
Mbadala kutoka NMB Benki Bw.George Kivaria akimpongeza mshindi wa Kwanza wa
shindano la uwekezaji “DSE Scholar
Investment Challenge” Bw. Laurent Amos
Dyanko mara baada ya kuibuka mshindi wa kwanza wa shindano hilo leo jijini Dar
es Salaam.
Katikati ni mshindi wa kwanza wa shindano la Uwekezaji “DSE Scholar Investment Challenge” akionyesha zawadi yake ya fedha taslimu shilingi 1000,000/= aliyozawadiwa mara baada ya kuibuka mshindi katika shindano hilo.Zawadi nyingine iimetolewa kwa mshindi wa pili ambapo amepata shilingi 600,000/= na mshindi wa tatu shilingi 400,000/=Shindano hilo lilianzishwa na DSE tarehe 1 April 2014 kwa lengo la kutoa elimu juu ya uwekezaji kwa njia ya kununua na kuuza hisa na kushirikisha wanafunzi wa vyuo vikuu hapa nchini ambapo jumla ya washiriki 5000 walijitokeza na hatimaye wakapatikana 50 ambao waliendelea na mchujo na kufikia tamati ya kupata washindi watatu. Kutoka kushoto ni Mwakilishi wa NMB Benki Bw. George Kavaria, Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana Bibi. Nasama Massinda, Afisa Mtendaji Mkuu wa DSE Bw. Moremi Marwa na Mkurugenzi wa Ufundi wa FSDT Bw. Sosthenes Kewe.
Mwakilishi wa NMB Benki, Bw. George Kivaria (wa pili kutoka
kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na washindi wa Shindano la Uwekezaji “DSE Scholar Investment Challenge” wakati wa
hafla ya kukabidhi zawadi kwa washindi wa shindano hilo leo jijini Dar es
Salaam.Kutoka kushoto ni mshindi wa kwanza Bw. Laurent Amos Dyanko, George
Firimin (mshindi wa pili) na Godlove Kellya mshindi wa tatu. (Picha zote na Frank Shija, Maelezo)








No comments:
Post a Comment