TANGAZO


Wednesday, August 13, 2014

HABARI MPASUKO: Msikiti wa Sheikh Ponda, Mtambani wateketea kwa moto sasa hivi


MSIKITI wa Mtambani (pichani), Kinondoni Dar es Salaam, unaotumiwa pia na Sheikh Issa Ponda unateketea kwa moto.

Kwa mujibu wa mmoja wa mashuhuda alisema kuwa msikiti huo uliochini ya umiliki wa Shura ya Maimamu, ambao pia Sheikh Ponda huutumia katika harakati zake za kudai haki za waislamu, ulianza kuungua eneo la paa majira ya saa 12;30 jioni hii.

Juhudi za kuuzima moto huo zilikuwa zinaelekea kushindikana kutokana kwa vile  paa lililoanza kuungua liko juu ya ghorofa.

Mpaka hivi sasa chanzo cha moto huo hakijaweza kupatikana.

Tutaendelea kuwaletea habari zaidi kadri tutakavyokuwa tunazipata.

No comments:

Post a Comment