TANGAZO


Monday, August 18, 2014

Redds Miss Tanzania yapata mdhamini mpya wa mavazi

Mkurugenzi wa Kampuni ya Lino Agency, waandaaji wa shindano la Redds Miss Tanzania, Hashim Lundenga, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, alipokuwa akitangaza udhamini wa Kampuni ya mavazi ya S&D Collection kwenye shindano hilo, kwa mwaka 2014. Kulia ni Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Devota Kijogoo na katikati ni Mkurugenzi mwenza, Esta Maro. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Mkurugenzi wa Kampuni ya mavazi ya S&D Collection, Devota Kijogoo, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, wakati kampuni yake hiyo, ilipotangaza udhamini wake kwa mashindano ya kumsaka Mrembo wa Redds Miss Tanzania 2014. Kushoto ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Lino Agency, waandaaji wa shindano hilo, Hashim Lundenga na katikati ni Mkurugenzi mwenza wa S & D Collection, Esta Maro. 
Mkurugenzi wa Kampuni ya mavazi ya S&D Collection, Devota Kijogoo, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, wakati kampuni yake hiyo, ilipotangaza udhamini wake kwa mashindano ya kumsaka Mrembo wa Redds Miss Tanzania 2014. Kushoto ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Lino Agency, waandaaji wa shindano hilo, Hashim Lundenga na katikati ni Mkurugenzi mwenza wa S & D Collection, Esta Maro. 

Habari za asubuhi,
Kwanza kabisa napenda kuchukua fursa hii kuishukuru kampuni ya Lino International agency Ltd, kupitia Mkurugenzi wake bwana Hashim Lundenga kukubali Kampuni yetu ya S & D Collection kuwa mmoja wa Wadhamini mwenza wa Mashindano makubwa kabisa ya urembo hapa nchini, Mashindano ya Redds Miss Tanzania, 2014.

S & D Collection ni Wakala wa DSTV, MAXCOM, CRDB kupitia Fahari Huduma. Pamoja na kuuza nguo ( BOUTIQUE) pia tunatoa huduma mbalimbali zikiwemo, Kulipia bili za maji – DAWASCO, kununua LUKU, Kulipia road licence,  kuunganisha wateja wapya na kulipia bills – DSTV. Kwa kupitia Fahari Huduma ya CRDB wateja wa CRDB wanaweza kutoa au kuweka pesa kwenye akaunti zao, kulipia ada za shule, Kufanya malipo wanaponunua bidhaa zetu na  pia kufungua akaunti za watu binafsi (Personal Account).

Dhumuni kubwa la Kampuni yetu kuingia katika mashindano haya ni kujitangaza. Kutangaza biashara ya mavazi, Bidhaa zetu tunaleta toka Marekani, Uturuki, Ghana na Ethiopia. Kwa kupitia jukwaa la Miss Tanzania naamini kwamba wananchi wataona bidhaa zetu na kuvutiwa nazo na hatimae kuja kwenye maduka yetu kununua, jambo ambalo ndilo kusudio kubwa la Kampuni yetu.
Katika kujihusisha na mashindano ya urembo ya Redds Miss Tanzania 2014 kampuni yetu itatoa mavazi ya aina mbalimbali kwa warembo wanaoshiriki mashindano haya. Mavazi hayo ni kuanzia mavazi kwa ajili ya show ya ufunguzi. Mavazi ya ubunifu kwa ajili ya washiriki kujitambulisha. Mavazi ya ufukweni, [beach wear] pamoja na mavazi ya jioni kwa washiriki watakaobahatika kuingia katika Tano bora, [Top 5] ya Redds Miss Tanzania 2014.

Kama hiyo haitoshi, tunakusudia pia kumpatia mavazi ya jioni mrembo wa Taifa atakayeshinda, ambae ndiye atayekuwa mwakilishi wa Nchi yetu kwenye mashindano ya urembo ya Dunia, kama nilivyofahamishwa mashindano hayo yatakuwa mwakani 2015.
Hivyo basi sina mengi ya kusema bali ni hayo tu, S & D Collection ipo Shoppers Plaza eneo la Mikocheni- tuko Gorofa ya pili., na lingine lipo katikati ya jiji - Pamba road , Karibuni kununua nguo na kupata huduma mbalimbali nilizozitaja hapo awali.
Karibuni sana na asanteni sana kwa kunisikiliza.

DEVOTA KIJOGOO MTAMBO.
MKURUGENZI
S & D COLLECTION.

No comments:

Post a Comment