TANGAZO


Monday, August 18, 2014

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dk. Rehema Nchimbi afungua jengo la huduma kwa wagonjwa wa nje (OPD) kwenye kituo cha Afya cha Lumumwa Mpwapwa

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk. Rehema Nchimbi akifungua kitambaa kuashiria ufunguzi wa jengo la huduma kwa wagonjwa wa nje (OPD), kwenye kituo cha afya cha Lumuma, Mpwapwa mwishoni mwa wiki. Jengo hilo, linalomilikiwa na Kanisa Katoliki Dodoma kupitia Shirika lake la Watawa la Mt. Gema, lina thamani ya sh. milioni 350. Kushoto ni Mkuu wa shirika hilo, Sister. Florencia Mbeyu.
Mkuu wa Mkoa Dodoma, Dk. Rehema Nchimbi akikata utepe kufungua jengo la huduma kwa wagonjwa wa nje (OPD), kwenye Kituo cha Afya cha Lumuma, Mpwapwa mwishoni mwa wiki. Kushoto  ni Mkuu wa Wilya ya Mpwapwa, Christopher Kangoye na kulia ni Bw. Anjelo Dauria, Mwenyekiti wa Shirika la Marafikii wa Lumuma la Italia, waliofadhili sh. milioni 350  za ujenzi wa jengo hilo. Kituo cha Lumuma, Mpwapwa kinamilikiwa na Kanisa Katoliki Dodoma kupitia shirika lake la watawa la Mt. Gema.
Muonekano wa jengo la huduma kwa wagonjwa wa nje (OPD), kwenye kituo cha Afya cha Lumuma, Mpwapwa, lililogharimu sh. milioni 350 kwa ufadhili wa Shirika la marafiki wa Lumuma la Italia. Jengo hilo lina idara zote muhimu zinazohitajika kwa ajili ya wagonjwa wa nje, lilifunguliwa mwishoni mwa wiki na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk. Rehema Nchimbi.
Muonekano wa jengo la huduma kwa wagonjwa wa nje (OPD), kwenye kituo cha Afya cha Lumuma, Mpwapwa, lililogharimu sh. milioni 350 kwa ufadhili wa Shirika la marafiki wa Lumuma la Italia. Jengo hilo lina idara zote muhimu zinazohitajika kwa ajili ya wagonjwa wa nje, lilifunguliwa mwishoni mwa wiki na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk. Rehema Nchimbi.
Mkuu wa Mkoa Dodoma, Dk. Rehema Nchimbi (kulia) akiserebuka kwa muziki wa kwaito, kusherehekea na baadhi ya vijana wa Kata ya Lumuma, Mpwapwa, waliojitokeza kwenye hafla ya ufunguzi wa jengo la huduma kwa wagonjwa wa nje (OPD), kwenye kituo cha Afya cha kata hiyo, mwishoni mwa wiki.
Hafla ya ufunguzi wa jengo jipya la huduma kwa wagonjwa wa nje (OPD), kwenye Kituo cha Afya cha Lumuma, Mpwapwa, iliyofanyika mwishoni mwa wiki, ilitanguliwa na Ibada takatifu iliyoongozwa na Makamu wa Askofu wa Kanisa Katoliki, Dodoma, Padiri Chesco Msaga (wa pili kulia). Kituo hicho cha Afya kinamilikiwa na kanisa hilo, kupitia shirika lake la Watawa la Mt. Gema.
Mkuu wa Mkoa Dodoma, Dk. Rehema Nchimbi akiwa amembeba mtoto aliyepewa jina lake la Rehema na mama yake, kama ishara ya kumuenzi mkuu huyo wa mkoa kwa kuwa mtoto huyo, alizaliwa kwenye kituo hicho cha Lumuma, Mpwapwa, majira ambayo mkuu huyo wa mkoa alikuwa ndio anawasili kituoni hapo kufungua jengo la huduma kwa wagonjwa wa nje (OPD), lililogharimu kiasi cha sh. milioni 350, mwishoni mwa wiki.
Picha ya pamoja kati ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, viongozi wa Kanisa Katoliki na Shirika la Watawa la Mt. Gema, Dodoma na marafiki wa Lumuma, raia kutoka Italia waliofadhili ujenzi wa jengo la wagonjwa wa nje (OPD), kwenye kituo cha afya cha Lumuma, Mpwapwa, wakati wa hafla ya ufunguzi wa jengo hilo, mwishoni mwa wiki.
Umati wa wananchi wa Kata ya Lumuma, Mpwapwa na maeneo ya jirani ya Wilaya ya Kilosa, Morogoro waliojitokeza kwenye hafla ya ufunguzi wa jengo la huduma kwa wagonjwa wa nje (OPD), kwenye Kituo cha Afya cha Kata ya Lumuma, Mpwapwa, mwishoni mwa wiki. (Picha zote na John Banda, Dodoma)

No comments:

Post a Comment