Rais wa Colombian Juan Manuel Santos amesema kuwa anaunga mkono matumizi ya bangi kwa minajili ya utabibu.
Bwana Santos ameunga mkono mswada ambao utapigiwa kura bungeni wakati wowote kwa manufaa ya kupunguza uchungu kwa wagonjwa .Colombia ni moja kati ya mataifa ambayo yamekumbwa na vita vya walanguzi wa madawa ya kulevya na serikali vita ambavyo vimesababisha mauaji ya mamia ya watu. .
Marijuana inakuzwa kwa wingi nchini Colombia, lakini taifa hilo linajulikana kote duniani kwa ukuaji wa cocaine, kwa pamoja na Peru.
"natumai tutaliangazia jambo hili la matumizi ya marijuana kwa mtazamo mpya utakaofaidi wagonjwa ambao wanaitegemea kupunguza uchungu.'' alisema bwa Santos akiwa mjini Bogota.
No comments:
Post a Comment