Baadhi ya ndugu na wageni mbalimbali waliohudhuria katika hafla ya kuwaapisha Majaji 20 wa Mahakama Kuu Tanzania, viwanja vya Ikulu, Dar es Salaam leo. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Baadhi ya Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama wakiwa katika hafla ya Rais Jakaya Kikwete kuwaapisha Majaji wa Mahakama Kuu Tanzania, Ikulu Dar es Salaam leo.
Baadhi ya Majaji waliokula kiapo cha utii kwa Rais na Jamhuri ya Muungano katika kulitumikia Taifa katika kazi ya Ujaji wa Mahakama Kuu Tanzania, Ikulu Dar es Salaam leo.
Rais Jakaya Kikwete, akimwapisha aliyekuwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), Elieza Felesh, kuwa Jaji wa Mahakama Kuu Tanzania, viwanja vya Ikulu Dar es Salaam leo. Rais Kikwete aliwaapisha majaji 20 wa Mahakama Kuu aliowateu katikati ya wiki iliyopita.
Rais Jakaya Kikwete, akimwapisha Winefrida Koroso kuwa Jaji wa Mahakama Kuu Tanzania, Ikulu Dar es Salaam leo. Rais Kikwete aliwaapisha majaji 20 wa Mahakama Kuu aliowateua katikati ya wiki iliyopita.
Rais Jakaya Kikwete, akimkabidhi vitendea kazi Winefrida Koroso baada ya kumwapisha kuwa Jaji wa Mahakama Kuu Tanzania, Ikulu Dar es Salaam leo.
Rais Kikwete, akimwapisha Mohamed Rashid kuwa Jaji wa Mahakama Kuu Tanzania, wakati wa hafla, iliyofanyika kwenye viwanja vya Ikulu jijini leo.
Rais Jakaya Kikwete, akimwapisha Amour Said kuwa Jaji wa Mahakama Kuu Tanzania katika hafla iliyofanyika viwanja vya Ikulu jijini leo.
Rais Jakaya Kikwete, akimkabidhi vitendea kazi Jaji Amour Said baada ya
kumwapisha kuwa Jaji wa Mahakama Kuu Tanzania, viwanja vya Ikulu jijini
leo.
Rais Kikwete (katikati mstari wa mbele), akipiga picha ya kumbukumbu na Majaji 20 wa Mahakama Kuu Tanzania mara baada ya kuwaapisha, viwanja vya Ikulu, jijini leo. Wapili kushoto ni Jaji Mkuu wa Tanzania, Mohamed Chande Othman na wakwanza ni Jaji Mkuu wa Zanzibar, Omar Othman Makungu.
Rais Kikwete, akipiga picha ya kumbukumbu na Jaji Salma Mussa Magimbi (kulia kwake) pamoja na familia yake, mara baada ya kuwaapisha majaji 20 wa Mahakama Kuu, Ikulu leo. Watatu kulia ni mama wa jaji huyo, Mbunge mstaafu kupitia Chama cha Wananchi (CUF), Mama Fatuma Magimbi.
Rais Jakaya Kikwete akipiga picha na mtangazaji wa TBC1, Grace Kingarame Kihampa, wakati wa hafla ya kuwaapisha Majaji wa Mahakama Kuu Tanzania, Ikulu Dar es Salaam leo.
No comments:
Post a Comment