Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein (katikati), akifuatana na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Serikali ya Muungano, Dk. Seif Rashid (kushoto), na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo, alipowasili katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro, mkoani Arusha leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein akisalimiana na Viongozi, wakati alipowasili katika jengo la Ofisi za Jumuiya ya nchi za Afrika ya Mashariki mjini Arusha leo, alipowasili kufungua mkutano wa Jumuiya ya Apecsa kwa kanda Mashariki, Kati na Kusini mwa Bara la Afrika.
Washiri wa Mkutano wa siku tatu wa Jumuiya ya Apecsa kwa kanda Mashariki, Kati na Kusini mwa Bara la Afrika wakimasikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein (hayupo pichani), wakati wa ufunguzi wa mkutano huo iliofanyika katika ukumbi wa jengo la Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein akiteta na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Serikali ya Muungano, Dk. Seif Rashid wakati wa Mkutano wa Jumuiya ya Apecsa kwa kanda Mashariki, Kati na Kusini mwa Bara la Afrika uliofanyika leo, katika ukumbi wa mikutano wa Jengo la Jumuiya ya Afika ya Mashariki, Mjini Arusha.
Washiri wa Mkutano wa siku tatu wa Jumuiya ya Apecsa kwa kanda Mashariki, Kati na Kusini mwa Bara la Afrika wakimasikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein (hayupo pichani), wakati wa ufunguzi wa mkutano huo, iliofanyika katika ukumbi wa jengo la Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein akizungumza na wajumbe wa Mkutano wa Jumuiya ya Apecsa kwa kanda Mashariki, Kati na Kusini mwa Bara la Afrika katika ukumbi wa mikutano wa Jengo la Jumuiya ya Afika ya Mashariki Mjini Arusha leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein akizungumza na wajumbe wa Mkutano wa Jumuiya ya Apecsa kwa kanda Mashariki, Kati na Kusini mwa Bara la Afrika katika ukumbi wa mikutano wa Jengo la Jumuiya ya Afika ya Mashariki, Mjini Arusha leo.
N a Richard Mwangulube, Arusha
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohamed Shein amezitaka nchi za Afrika ya Mashariki, Kati na kusini kuimarisha zaidi masuala ya uchunguzi hususani uchunguzi wa maradhi yanatowakabili binadamu.
Rais Shein amesisitiza kwamba ushirikiana katika kukabiliana na mardhi ni jambo la msingi katika nchi hizi.
Rais Shein ametoa wito huo wakati akifungua mkutano wa siku tatu wa watalaam wa sekta ya afya kutoka nchi za afrika ya mashaiki, kati na kusini unaofanyika kwenye ukumbi wa Jumuiya ya Afrika ya Mashriki Mkoani Arusha leo.
Mwenyekiri huyo amewambia watalaam hao kwamba mkutano huo wakati sekta ya afya inakabiliwa na changamoto nyingi katika uchunguzi wa maradhi
Amesisitiza kwamba nchi hizo lazima ziimarishe eneo la maabara ambayo ambalo ni muhimu zaidi katika uchunguzi wa maradhi katika nchi hizo
Amesema ni jambo muhimu kuhakikisha maabara zinakua na vifaa vya kisasa pamoja na menejimenti yenye utaalam wa hali ya juu ili kuweza kuchunguza magonjwa mbalimbali yakiwemo ya kansa kwa umakini na uhakika zaidi.
Rais Shein amesema ubora wa menejimenti na mfumo mzima wa maabara ni eneo ambalo linapaswa kuepewa umuhimu wa pekee.
Amesema madaktari hawezi kutoa matibabu mazuri bila maabara kutoa uchunguzi wa uhakika.
Amezitaka nchi hizo kuandaa mikakati imara ya kuwa na maabara bora zenye vifaa vya kisasa ili ziwawezesha watalaam wa patholojia kutoka kufanya uchunguzi wa uhakika.
Amesisitiza umuhimu wa nchi hizo kuboresha zaidi maabara ili ziweze kutoa huduma bora zaidi.
Pia ametilia mkazo suala la mafunzo kwa watalaam wa patholojia katika ukanda huu wa afrika.hili ni muhimu kwa waandaji mipango.
Amesema nafasi ya maabara katika kuchunguza maradhi ni muhimu.
Hivyo ametaka kuwepo na mikakati thbiti kwa ajili ya kuboresha maabara na huduma mbalimbali za afya katikanchi hizi.
Akizungumza katika mkutano huo mwenyekiti wa chama cha wataalam wa APESCA Dkt Edda Vuhahula amesema huu ni mkutano wa 12 wa wataalam wa eneo la maabara kwa nchi hizi nan i mkutano wa wanasayansi wanaohusika na uchunguzi wa mardhi katika maabara.
Dkt Vuhahula amefafanua kuwa wataalam hao watangalia nafasi ya maabara katika kukabiliana na maradhi na watabadilishana uzoefu kati ya nchi hizi.
Pia watangalia changamito zinazokabili eneo la maabala katika utoaji wa huduma bora za afya na tafiti za kisanyansi kusiana na changamoto zilizopo amefafanua Dkt Vuhahula.
Akizungumza katika mkutano huo Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt Seif Rashid amesema wajibu wa sekta ya maabara kaika kutoa huduma bora za afya.
Aidha Dkt Seif Rashid amesisitiza kwamba huduma za afya kamwe haziwezi kuboreshwa bila ubora wa huduma za maabara
Amesisitiza kuwa bila kuwepo na vipimo sahihi kupatikana matibabu hata hivyo hali ya maabara nchini zimeborashwa kwa kiwango cha juu kutokana na utoaji wa huduma bora pamoja na kuwepo na vifaa vya kisasa vya uchunguzi wa maradhi katika Mikoa na Wilaya zote.
No comments:
Post a Comment