TANGAZO


Monday, July 7, 2014

Vodacom Foundation yafuturisha yatima Zanzibar

Mgeni rasmi kwenye hafla ya kufuturisha  watoto waishio katika mazingira magumu mjini Zanzibar,Kadhi Mkuu wa Zanzibar,akiwasili kwenye hafla hiyo iliyoandaliwa na Vodacom Foundation na kupokewa na Meneja wa Vodacom tawi la Zanzibar, Mohamed Mansoor.
Baadhi ya watoto wanaoishi katika mazingira magumu mjini Zanzibar wakimsikiliza Kadhi Mkuu Zanzibar Khamis Haji alipokuwa anazungumza nao wakati wa hafla ya kufuturisha watoto hao iliyoandaliwa na Vodacom Foundation jana.
Kadhi Mkuu wa Zanzibar akikabidhi vyakula, mbuzi, mafuta, mchele na  madaftari kwa watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi mjini Zanzibar kwa niaba ya Vodacom Foundation,Wakati wa hafla ya kufuturu hapo jana, Anaeshuhudia kushoto ni Meneja wa Vodacom Tanzania tawi la Zanzibar Mohamed Mansoor.
Viongozi wa dini mjini Zanzibar pamoja  na wa Vodacom Tanzania wakiongozwa na mgeni rasmi Kadhi wa Zanzibar Khamis Haj wakipata futari katika  hafla hiyo iliyoandaliwa na Vodacom Foundation kwaajili ya watoto waishio katika mazingira hatarishi mjini Zanzibar.
Kadhi Mkuu wa Zanzibar, Khamis Haj akihutubia kwenye hafla ya kufuturisha watoto wanaoishi katika mazingira magumu mjini Zanzibar,Hafla hiyo iliandaliwa na Vodacom Foundation.
Juma Haji mkazi wa Zanzibar akisaidia kuwagawia Maji na vyakula baadhi ya watoto waishio katika mazingira magumu waliohudhuria hafla ya kufuturu iliyoandaliwa na Vodacom Foundation kwaajili yao hapo jana.

No comments:

Post a Comment