TANGAZO


Tuesday, July 8, 2014

Pistorius:Mashahidi walikataa kutoa ushahidi


Baadhi ya mashahidi katika kesi inayomkabili mwanariadha wa Afrika Kusini Oscar Pistorius, walikataa kutoa ushahidi katika kesi hiyo kwa hofu ya kuoenakana hadharani.
Hii ni kwa mujibu wa wakili wa Pistorius.
''Hawakutaka sauti zao kusikika kote duniani, '' alisema wakili Barry Roux, huku akimaliza kuwasilisha kesi yake kwa mahakama.
Mahakama imeahirisha kesi hiyo hadi tarehe 7 Agosti.
Mwanariadha huyo , amekanusha madai ya kumuua kwa maksudi Reeva Stinkamp , akisema kuwa alidhani alikuwa jambazi.
Upande wa mashitaka, unamtuhumu Pistorius kwa kumuua Steenkamp kwa maksudi baada ya wawili hao kutofautiana.
Ingawa upande wa mashitaka umesema kuwa mashahidi walikataa kutoa ushahidi, huenda isiathiri kwa vyovyote ushahidi wake kwani uzito wa kesi yake inategemea sana ushahidi wake na ule wa wataalamu.
Dunia ilisikia usimulizi wa mauaji ya Reeva Steenkamp alipoanza kutoa ushahidi kuanzia Aprili.
Tangu hapo, upande wa mashitaka umetaka kuonyesha mahakama kuwa mauaji hayo yalikuwa ajali.
Wataalamu wao walitoa maelezo kuhusu hali yake ya kiakili na ambavyo iliathiri ulemavu wake.

No comments:

Post a Comment