*Serikali kutumia trioni 19.853.3
*Bei ya Vileo kupanda
*Ya Pembejeo kushuka
*Wafanyakazi wapata nafuu ya kodi
Waziri wa Fedha, Saada Mkuya Salum, akionesha mkomba wenye Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2014/15, nje ya viwanja vya Bunge wakati akielekea kwenye ukumbi wa Bunge kwa ajili ya kuiwasilisha leo, mjini Dodoma.
*Bei ya Vileo kupanda
*Ya Pembejeo kushuka
*Wafanyakazi wapata nafuu ya kodi
Waziri wa Fedha, Saada Mkuya Salum, akionesha mkomba wenye Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2014/15, nje ya viwanja vya Bunge wakati akielekea kwenye ukumbi wa Bunge kwa ajili ya kuiwasilisha leo, mjini Dodoma.
Na mwandishi wetu, Dodoma
WAZIRI wa
Fedha, Saada Mkuya Salum, leo amewasilisha Bajeti ya sh. trioni 19.853.3 kwa ajili ya matumizi ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2014/2015, huku lengo likiwa kuongeza makusanyo ya mapato kwa kuanzisha vyanzo vipya,
kuboresha vilivyopo na kupunguza misamaha ya kodi.
Waziri wa
Fedha, Saada Mkuya ameliambia Bunge kuwa bajeti hiyo imelenga kupunguza gharama
za maisha ya wananchi kwa kuendelea na jitihada za kudhibiti mfumuko wa bei,
kuendelea kuboresha huduma za jamii na kuboresha miundombinu ikiwemo ya
barabara na umeme.
“Aidha
bajeti hii imezingatia pia maandalizi ya Katiba mpya, uchaguzi wa Serikali za
Mitaa na maandalizi ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2015,”alisema Mkuya.
Waziri huyo
alibainisha pia bajeti hiyo, imelenga kuongeza upatikanaji wa nishati ya umeme
wa uhakika, kuboresha elimu, kuunganisha nchi kwa njia ya miundombinu ya
barabara, reli na viwanja vya ndege.
Waziri huyo
wa Fedha alisema Serikali imepanga kushughulikia kwa nguvu zaidi kero mbalimbali
zinazowakabili wananchi zikiwemo upatikanaji wa maji, nishati ya uhakika, elimu
kuhusu umuhimu wa faida za kulipa kodi kwa kutumia mitandao ya kieletroniki na
kusiamia ulipaji kodi kwa hiari kupitia udhibiti wa matumizi ya mfumo wa
mashine za kieletroniki za kutoa risiti ambao umeboreshwa zaidi.
Aidha, alisema
ili kuleta ufanisi katika usimamizi wa bajeti, Serikali inaandaa muswada wa
sheria ya bajeti ambao utaletwa bungeni mwaka huu.
Alisema
katika kipindi hicho bajeti hiyo itatekeleza utoaji wa fedha kwa mafungu utakaozingatia
uwasilishaji wa taarifa za matumizi ya kawaida na maendeleo kwa kila robo ya
mwaka sanjari na kuwianisha pamoja na kuandaa sheria ya bajeti.
Aidha
alisema mgawanyo wa fedha katika bajeti hiyo umewekewe kipaumbele katika sekta
ya nishati na madini ambapo imetengewa asilimia 7 ya bajeti yote ya Serikali.
Kipaumbele
kingine kimekwenda katika sekta ya miundombinu ya usafirishaji ambapo
imetengewa sh. trioni 2.10 ambapo sh. bilioni 179 ni kwa ajili ya ununuzi wa
mabehewa na ukarabati wa reli ya kati na nyingine huku trioni 1.414 kwa ajili
ya ujenzi na ukarabati wa barabara na madaraja.
“Azma hii
inalenga kupunguza msongamano wa magari mijini, gharama za usafiri na
usafirishaji wa bidhaa na huduma na hivyo kupunguza mfumuko wa bei,”alisema.
Mkuya
alisema sekta nyingine iliyopewa kipaumbele katika bajeti hiyo ni kilimo ambapo
sh. trioni 1.084 zimetengwa kwa ajili ya kuimarisha miundombinu ya umwagiliaji
katika maeneo mbalimbali yakiwemo ya SAGCOT, ujenzi wa maghala na masoko.
Hali kadhalika
Elimu nayo imetengewa asilimia 23 ya bajeti ya Serikali ambapo vipaumbele
vimewekwa katika kuimarisha ubora wa elimu ikijumuisha miundombinu ya elimu
hatua ambayo itasaidia upatikanaji wa vifaa vya kujifunzia na kufundishia
sanjari na kuimarisha ikiwemo ni pamoja kujenga madarasa na maabara.
Alisema ili
kuhakikisha vijana nchini wanapata fursa za ajira, juhudi zitawekwa kwenye
kuimarisha vyuo vya ufundi stadi (Veta).
Maeneo
mengine ni maji, afya na utawala bora ambapo Serikali imetenga sh. bilioni
579.4 kwa ajili ya kuimarisha utawala bora ikijumuisha kugharamia Bunge Maalum
la Katiba, vitambulisho ya taifa, uchaguzi wa serikali za mitaa wa mwaka 2014,
kuhuisha daftari la wapiga kura, maandalizi ya uchaguzi mkuu mwakani na
mapambano dhidi ya rushwa.
Aidha ili
kuongeza mapato ya Serikali na kufikia malengo ya kiuchumi katika mwaka
2014/2015 wizara hiyo imependekeza kufanyiwa marekebisho ya mfumo wa kodi na
tozoikiwemo kurekebisha kodi chini ya sheria mbalimbali na pia taratibu za
ukusanyaji na usimamizi wa mapato ya Serikali.


No comments:
Post a Comment