TANGAZO


Wednesday, June 11, 2014

Taasisi ya Kiislamu ya Ahmadiyya yatumia sh. mil. 109 kusaidi maji vijijini

Mtoto mkazi wa Kijiji cha Ibihwa, wilayani Bahi, akikinga maji yanayotoka katika bomba la kisima cha kupampu kwa furaha kutokana na kukosa maji kwa muda mrefu kutokana na bomba la kisima hicho kuharibika kabla ya kutengenezewa tena kwa msaada wa Taasisi ya Kiislamu ya Ahmadiyya Jamaat.
Mwananchi wa Kijiji cha Ibihwa, wilayani Bahi, akikinga maji yanayotoka katika bomba la kisima cha kupampu kwa furaha kutokana na kukosa maji kwa muda mrefu kutokana na bomba la kisima hicho kuharibika kabla ya kutengenezewa tena kwa msaada wa Taasisi ya Kiislamu ya Ahmadiyya Jamaat.
Wananchi wa kijiji cha Kitumbili kilichopo Singida wakiangali maji yanayotoka katika bomba la kisima cha kupampu mara baada ya kukamilika matengezo yake na kukabidhiwa kwa ajili ya matumizi, ambapo ukarabati wa kisima hicho kilichokuwa kimejifukia ulifanya na Taasisi ya Kiislam ya Ahmadiyya Jamat inayojishuhulisha na huduma za kijamii.

Sheikhe wa Mikoa ya Kanda ya Kati kwa Mikoa ya Dodoma na Singida  wa Jumuiya hiyo, ya Waisilam Waahmadiyya Tanzania Bashart ur Rehman Butt, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari. (Picha zote na John Banda)

Na John Banda, Dodoma.
WANANCHI wa Vijiji mbalimbali vya Tanzania Bara na Visiwani ambavyo havikuwa na maji kwa muda mrefu, wamepata neema hiyo, baada ya kuchimbiwa, kujengewa na kukarabatiwa visima vya maji vya zaidi ya shilingi  milioni 109 na taasisi ya Kiisilam ya Ahmadiyya Jamaat inayojishughulisha na huduma za kijamii.
Sheikhe wa Mikoa ya Kanda ya Kati kwa Mikoa ya Dodoma na Singida  wa Jumuiya hiyo, ya Waisilam Waahmadiyya Tanzania Bashart ur Rehman Butt, alisema kuwa kati ya visima hivyo vilivyochimbwa vipya ni 20 na vilivyokarabatiwa 25.

Alibainisha kuwa visima vipya 20 walichimba na kujenga kwa kiasi cha sh. milioni 94.5 na visima 25, vilivyofanyiwa ukarabati vilighalimu sh. 15 milioni ambayo jumla ni sh. 109.5 mil. wakiwa na lengo la kuwasaidia kuondokana na kero hiyo ya ukosefu wa maji katika vijiji hivyo ambavyo akina mama walikuwa wanatafuta maji kwa umbali wa km zaidi 6.
 
Alisema pamoja na maji hayo kufuatwa mbali bado walikuwa
wakishirikiana kwa matumizi na mifugo huku wanafunzi wa shule zilizopo katika vijiji hivyo kulazimika kwenda mashuleni na maji bila kujali umbali walikokuwa wanatoka.

“Chakusikitisha zaidi vijiji vingi vilivyosaidiwa tumekuta wakazi wake wanatembea mwendo mrefu kusaka maji safi na salama na hata hivyo maji hayo yanatuwa na mifugo huku wanafunzi wakilazimishwa kufika na maji mashuleni”alisema.
 
Aidha, Rehman Butt alisema kati ya visima, vilivyokarabatiwa miongoni mwake, vipo vinavyomilikiwa na Serikali na vinavyo simamiwa na Jumuiya ya Ahmadiyya Tanzania.

Sheikhe huyo hata hivyo alisema kuwa pamoja na uchimbaji na ukarabati wa visima pia jumuiya imejiwekea mkakati ya kuwawekea mfumo wa Solor kwa wananchi wa vijijni, ambao hawatarajii kuipata nishati hiyo ya umeme, kuanzia mwaka mpya wa fedha utakaoanza Julai mwaka huu.

Aidha, alisema kwa mikoa ya Dodoma na Singida tayari baadhi ya vijiji vimekarabatiwa  visima vyao ambavyo vilikuwa vimekufa na kujengewa vipya.

Alitaja vijijii hivyo ambavyo na idadi yake kwenye mabano ni Ng’ambi (2) Kitumbili (2) na Kinyeto (1) vyote vya Mkoa wa Singida kwa upande wa Mkoa wa Dodoma ni  vijiji vya Kigwe (2) Ibiwa (2) ambavyo hata hivyo vilikuwa vimekufa.

Jumuia hiyo iliyoingia kwa mara ya kwanza nchini mwaka 1935 kwa lengo la kuisaidia jamii katika maeneo ya Maji, Afya na Elimu kauli mbiu yao ni Upendo kwa Wote, Chuki si kwa Yeyote.


No comments:

Post a Comment