Sehemu ya mto Nile ambapo kando yake
ndiyo kuna Hoteli ambayo Waheshimiwa Mawaziri waliandaliwa chakula cha
jioni. Angani ni helikopta ikiwa katika doria kuhakikisha kuwa hakuna
mtu anadhurika.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb) kushoto akisalimiana na Waziri wa
Mambo ya Nje wa Misri, Mhe. Nabil Fahmy.
Mhe. Membe na Mhe. Fahmy walifanya
mazungumzo katika Hoteli aliyofikia Waziri Membe. Mazungumzo yao
yalihusu kuimarisha ushirikiano, Misri kurejea katika Umoja wa Afrika na
matumizi ya maji ya mto Nile.
Waziri Membe akiwa na Ofisa kutoka
Wizara ya Mambo ya Nje wa Misri, Bi. Fatma. Bi. Fatma ambaye alishawahi
kufanya kazi katika Ubalozi wa Misri nchini Tanzania ndio alikuwa Afisa
Itifaki anayemuhudumia Mhe. Waziri na ujumbe wake.
Waziri Membe akitoa neno la shukrani kwa
niaba ya Mawaziri wenzake baada ya kushiriki katika chakula cha jioni
kilicho andaliwa kwa heshima yao na Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri
Waziri Membe (kushoto) akiongea
na Msaidizi wa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri ambaye ana ngazi
ya Ukurugenzi kwenye chumba cha Wageni Maalum katika Uwanja wa Ndege wa
Cairo alipowasili kwa ajili ya kushiriki sherehe za kumuapisha Rais wa
nchi hiyo.
Waziri wa Mambo ya Nje (kulia) akipokea
taarifa fupi kutoka kwa Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Misri, Bw.
Jestas Nyamanga katika Hoteli aliyofikia Mhe. Waziri ya Fairmont.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb) (kulia) akiwa katiika Kiwanja cha
Ndege cha Addis Ababa akiwa njiani kuelekea Cairo, Misri katika
sherehe za kumuapisha Rais Mteule, Mhe. Abdel Fattah al Sisi. Mwingine
katika picha ni Bw, Shelukindo, Afisa wa Ubalozi wa Tanzania nchini
Ethiopia.
Mhe. Waziri Membe mwenye miwani akiwa
amesimama mbele ya Hoteli ili kuingia katika gari maalum kwa ajili ya
kumpeleka eneo lililofanyika sherehe za uapisho. Kulia kwake ni
Mkurugenzi wa Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa, Balozi Vincent Kibwana.
Balozi
Kibwana (kushoto) akijadili jambo na Afisa wake, Bw. Celestine
Kakere. (Picha zote na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa)

No comments:
Post a Comment