TANGAZO


Thursday, May 22, 2014

Zanzibar na China zatia saini makubaliano ya ujenzi wa ICU katika Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja mjini Zanzibar


Katibu Mkuu Wizara ya Afya Zanzibar, Dk. Mohammed Jidawi wa kwanza (kulia) na Meneja miradi wa kampuni ya Beijing Construction Engineering Mr. Qi  Xin (wakushoto) wakibadilishana hati ya makubaliano ya ujengwaji wa ICU mpya katika Hospitali Kuu ya Mnazi mmoja itayogharim dola za kimarekani milioni moja na laki moja ambazo dola mia nane na hamsini ni zavifaa.
(Picha na Makame Mshenga wa Maelezo Zanzibar).
 Balozi Mdogo wa China visiwani Zanzibar, Kie Yunliang (wakwanza kushoto) akishuhudia utiaji saini makubaliano ya ujenzi wa ICU,  kulia Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dk. Mohammed Jidawi na wakatikati ni Meneja miradi wa kampuni ya Beijing Construction Engineering Mr. Qi Xin ambayo ndiyo itakayojenga hafla hiyo imefanyika Wizara ya Afya.
Balozi Mdogo wa China visiwani Zanzibar, Kie Yunliang (watatu kushoto) akitoa maelezo kwa baadhi ya viongozi wa Wizara ya Afya waliongozwa  na Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dk.. Mohammed Jidawi kabla ya utiaji saini makubaliano ya ujengwaji wa ICU mpya ya kisasa itayojengwa Hospitali Kuu ya Mnazi mmoja.

No comments:

Post a Comment