Mbunge wa Sengerema mkoani Geita, William Ngeleja akizindua albamu ya Msaada Wangu wa Karibu ya Msanii Grace Mwikabwe wakati wa Tamasha la Injili kwenye uwanja wa CCM Kirumba. Wa kwanza kushoto ni Grace Mwikwabe na kulia ni Alex Msama.
Maaskofu, Wachungaji na mgeni rasmi, Mbunge William Ngeleja, wakishikilia albam ya Msaada Wangu wa Karibu kwa ajili ya kuiombea kabla ya kuznduliwa jana.
William Ngeleja akihutubia mamia ya watazamaji wa tamasha la muziki wa injlili.
Watazamaji wakifuatilia tamasha hilo.
Rose Mhando akiwarusha waatazamaji.
Watazamaji wakiwa katika tamasha hilo pamoja na familia zao.
Na Mwandishi wetu
MBUNGE wa Bunge Maalum la
Katiba,William Ngeleja, ameupigia debe Muziki wa Injili kuwa unayofasi ya kubwa
ya kuhubiri amani nchini mbali ya kuhubiri jamii kumtukuza na kumcha Mungu.
Alisema amani iliyopo nchini imejengwa
na watu wengi wakiwemo wasanii wa nyimbo za injili,Maaskofu,Wachungaji na watu
wengine wengi hivyo kwa pamoja tutazidi kuimarisha nchi yetu.
Alitoa kauli hiyo jana Jijini Mwanza
kwenye uwanja wa CCM Kirumba, kabla ya kuzindua albamu ya Msaada Wangu wa Karibu
ya msanii Grace Mwikwabe
“Alichofanya hapa msanii huyo ni
mchango mkubwa kwa amani ya Tanzania ambayo imejengwa na watu wengi.Hivyo Muziki
huu unayo nafasi kubwa ya kuhubiri amani hiyo,”alisema Ngeleja
Hata hivyo Waziri huyo wa zamani wa serikali
ya awamu ya nne,aliwashuruku Viongozi wa Kiroho kwa ushiriki wao wa kukubali
mpango wa Mungu,Mwanza kuwa eneo la kuhubiri amani, neno la Mungu na nyimbo za
kumhubiri Mungu,kwamba ni jambo jema kumwimbia Bwana.
Akizungumzia mchakato wa katiba alisema wabunge
hao wamelitia taifa aibu kubwa,kwa sababu ya njia kutokuwa nyeupe wala nyoofu
na akadai hakuna mafanikio bila kuwa na changamoto.
Alisema minyukano ndani ya Bunge
hilo la Katiba,isiwakatishe tamaa,lakini kwa maombi ya Viongozi wa dini,mchakato
huo utafika salama na hatimaye kujenga mazingira mazuri ya Watanzania kuwa na Katiba
nzuri.
“Sisi kama taifa katika kipindi hiki
kigumu cha kupatia utaratibu wa kuongoza nchi yetu,na utaratibu wa injili
kuhubiriwa na amani kuwepo.Bunge la Katiba tumelitia aibu kubwa taifa lakini hakuna
mafanikio bila kupitia changamoto mbalimbali,”alisema Ngeleja
No comments:
Post a Comment