Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Makame
Mbarawa (katikati) na Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Jenista
Muhagama, wakimsilikiza Ofisa Uhusiano wa Chuo cha Kikristo cha Uganda, Prim
Tumuramye baada ya ufunguzi wa Maonesho ya 9 ya Elimu ya Juu, Sayansi na
Teknolojia, yaliyoanza leo, kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee, jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Jenista Muhagama,
akimueleza jambo Naibu Mkuu wa Chuo cha Ualimu cha Dar es Salaam (DUCE) Profesa
Godliving Mtui (katikati) kwenye ufunguzi wa Maonesho ya 9 ya Elimu ya Juu,
Sayansi na Teknolojia yaliyoanza leo kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee. Kulia ni
Waziri wa Mawsiliano, Sayansi na Teknolojia Profesa Makame Mbarawa.
Mtaalamu wa Masuala ya Lishe kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo
cha Sokoine (SUA) Gaudensia Donati akimueleza jambo Waziri wa Mawasiliano,
Sayansi na Teknolojia Profesa Makame Mbarawa na Naibu Waziri wa Elimu na
Mafunzo ya Ufundi Jenista Muhagama (anayeonekana mikono),wakati walipotembelea
banda la chuo hicho.
Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Profesa
Makame Mbarawa, akiangalia aina za panya wanazalishwa na Chuo Kikuu cha Kilimo
cha Sokoine (SUA) katika Maonesho ya 9 ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia
yaliyoanza leo kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee.
Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Profesa
Makame Mbarawa, akimueleza jambo Makamu Mshauri wa Wanafunzi wa Shule ya
Kimataifa ya Elimu iliyoko chini ya Chuo Kikuu cha Syansi na Teknolojia cha
Huazhong cha nchini China, Annie Zhao wakati alipotembelea banda la chuo hicho.
Makamu Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Zanzibar, Profesa Idris
Rai akiwaonesha jambo Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Profesa
Makame Mbarawa (katikati) na Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Jenista
Muhagama, wakati walipotembelea banda la chuo hicho.
Ofisa Mitihani kutoka Baraza la Mitihani, Daniel Malemba
akiwaeleza jambo baadhi ya wanafunzi waliotembelea banda la baraza hilo
kwenye Maonesho ya 9 ya Elimu ya Juu,
Sayansi na Teknolojia yaliyoanza leo kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee.
Ofisa Uhusiano wa Chuo Kikuu cha Waislamu cha Morogoro Ally
Sadi, akizungumza na baadhi ya wanafunzi waliotembelea banda la baraza hilo
kwenye Maonesho ya 9 ya Elimu ya Juu,
Sayansi na Teknolojia yaliyoanza leo kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee.
Ofisa Mikopo Mwandamizi wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa
Elimu ya Juu(HESLB ), Josephat Bwathondi, akitoa maelezo kwa baadhi ya
wanafunzi waliotembelea banda la bodi hiyo kwenye Maonesho ya 9 ya Elimu ya Juu, Sayansi na
Teknolojia yaliyoanza leo kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee.
Mwanafunzi wa Mwaka wa kwanz wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha
Udaktari na Teknolojia (IMTU), akimpima ‘presha’ Emmanuel Suluba ambaye ni mmoja
wa wanafunzi walitembelea banda la chuo hicho ambapo vipimo hivyo vinatolewa
bure. (Picha zote na Hussein
Makame-MAELEZO)
No comments:
Post a Comment