Kamishna wa
Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012, Hajjat Amina Mrisho Said (kushoto), akiwaeleza waandishi wa habari hawapo (pichani), kuhusu uzinduzi wa chapisho la
Tatu la taarifa za Msingi za Kidemografia, Kijamii na Kiuchumi linalotokana na
Sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012, ambao utafanywa na Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, tarehe 25 Mei
2014 katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu J. K. Nyerere uliopo jijini
Dar es Salaam. Kulia ni Ofisa Habari wa Idara ya Habari Maelezo, Frank Mvungi. (Picha na Idara
ya Habari Maelezo)
Frank
Mvungi-Maelezo
RAIS wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya
Mrisho Kikwete anategemewa kuwa Mgeni rasmi katika uzinduzi wa Chapisho la Tatu la
Taarifa za msingi za Kidemografia, kijamii na kiuchumi
linalotokana na Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012 katika ngazi ya Taifa.
Hayo yamesemwa
na Kamishna wa Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012 Hajjat Amina Mrisho Said
wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam ambapo uzinduzi
huo utafanyika Mei 25, mwaka huu katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere
uliopo Dar es Salaam.
Hajjat Amina
alisema kwa kifupi chapisho hilo,
linatoa viashiria mbalimbali ambavyo ni pamoja na ongezeko la idadi ya
watu,mgawanyo wa watu kwa umri na jinsi,muundo wa kaya,hali ya ndoa,hali ya
ulemavu,idadi ya Watanzania wanaoishi nje ya nchi na wale wenye vyeti vya kuzaliwa na wasionavyo.
Alivitaja viashiria vingine ni vizazi na vifo,uhai wa
wazazi,kujua kusoma na kuandika,shughuli zaki uchumi,hali ya makazi,mifuko ya
hifadhi ya jamii na umiliki wa vifaa na huduma katika makazi.
Akifafanua zaidi
kuhusu siku hiyo Hajjat Amina amesema watu wapatao 500 wanatarajiwa kushiriki katika
uzinduzi huo wakiwemo viongozi wa ngazi za juu Serikalini,Mabalozi na Wadau wa
maendeleo.
Hajjat Amina aliongeza
kuwaViongozi wengine watakaoshiriki ni wa
Dini,vyama vya Siasa na Wawakilishi wa Mashirika yasiyo ya kiserikali Pamoja na
wadau wa Takwimu nchini.
Chapisho la Tatu
la Taarifa za Msingi za Kidemografia,kijamii na kiuchumi linalotokana na Sensa
ya watu na Makazi ya mwaka 2012 ni mwendelezo wa machapisho mbalimbali
yanayotolewa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu na Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali
ya Mapinduzi Zanzibar kama ilivyoainishwa kwenye kalenda ya machapisho ya Sensa
ya watu na makazi ya mwaka 2012.
No comments:
Post a Comment