TANGAZO


Friday, May 2, 2014

Waziri Mkuu Mizengo Pinda kesho kuzindua maadhimisho ya Wiki ya Elimu Dodoma

Msemaji wa Serikali Bw. Assah Mwambene akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani), kuhusu maadhimisho ya Wiki ya Elimu yatakayo fanyika Kitaifa mkoani Dodoma. Kulia ni Afisa Habari wa Idara ya Habari Magreth Kinabo.

Na Hassan Silayo- MAELEZO
WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Pinda kesho atazindua maadhimisho ya Wiki ya Elimu Mjini Dodoma.

Akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, Msemaji wa Serikali Bw. Assah Mwambene alisema kuwa Maadhimisho hayo yatakwenda sambamba na Maofisa Elimu wa Mikoa kutoa taarifa kwa wananchi kupitia vyombo vya habari kuhusu maendeleo ya sekta ya Elimu katika Mikoa yao.

“Maadhimisho ya Wiki ya Elimu yatakwenda sambamba kwa taarifa mbalimbali kuhusu mafanikio katika sekta ya elimu kutolewa na maafisa elimu wa mikoa ili kuwapa fursa wananchi kujua nini kimefanyika katika sekta ya elimu”. Alisema Mwambene.

Pia Bw. Mwambene aliongeza kuwa katika maadhimisho hayo shule mbalimbali za msingi na sekondari zilizofanya vizuri katika mitihani ya kitaifa zitapewa zawadi.

Aidha Mwambene aliongeza kuwa wanafunzi walioandika insha kuhusu Afrika Mashariki na SADC watapewa zawadi.


Maadhimisho hayo yatafungwa Tarehe kumi na Rais Jakaya Kikwete mkoani Dodoma.

RATIBA YA MIKUTANO YA WAANDISHI WA HABARI NA MAAFISA ELIMU WA MIKOA
S/N
TAREHE
MKOA
MHUSIKA
NAMBA YA SIMU
1
2/5/2014
DODOMA
BW.JUMA KAPONDA

0784 584863
MOROGORO
BIBI W. NKAYA

2
3/5/2014
DSM
BW. R. MAPUNDA
0754 744536
PWANI
BW. YUSUPH KIPENGELE

TANGA
BW. R. CHOMOLA

3
4/5/2014
KILIMANJARO
BIBI. LUCY MALISA

TABORA
BW. J. MABEYO

RUVUMA
BIBI. MAYASA HASHIM

4
5/5/2014
KATAVI
BW. ERNEST HINJU

RUKWA
BW. S. MGINA

LINDI
BW. GIFT ENOCK

MTWARA
BW. HIPSON KIPENYA

5
6/5/2014
MANYARA
BW. IBRAHIM MBANGO

NJOMBE
BW. SAID NYANSILO

MBEYA
BW. R. NTYAMA

ARUSHA
BW. NESTORY MLOKA

6
7/5/2014
MWANZA
BW. H. MAULID
0754 432691
MARA
BW. E. MPALILE

GEITA
BIBI. E. BUCHUMA

SIMIYU
BW. A. KAMAMBA
0764856644
7
8/5/2014
KIGOMA
BW. SALVATORY SHAURI
0754 361266
KAGERA


SHINYANGA
BIBI. EVA MLOPA

8
9/5/2014
IRINGA
BW. J. MNYIKAMBI

SINGIDA
BIBI. FATUMA KILIMIA


9

10/5/2014



No comments:

Post a Comment