TANGAZO


Thursday, May 29, 2014

Shirika la Posta Tanzania (TPC) laelezea mafanikio, malengo na majuku yake katika kuihudumia jamii

Meneja Masoko wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), David George, akifafanua jambo kwa waandishi, wakati uongozi wa shirika hilo, ulipokuwa ukizungumza nao, kuelezea pamoja na mambo mengine, kazi, majukumu, mafanikio na malengo ya shirika hilo, Dar es Salaam leo. Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano cha shirika, Elia Madules na kulia ni Kaimu Meneja Huduma za Barua, Jason Kalile. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Waandishi wa habari, wakiandika habari zilizokuwa zikitolewa na uongozi wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), wakati wa mkutano huo, jijini leo. Uongozi wa shirika hilo, ulikuwa ukielezea pamoja na mambo mengine, kazi, majukumu, mafanikio na malengo ya shirika hilo, katika kuihudumia jamii ndani ya nchi na Kimataifa.
Waandishi wa habari, wakiandika habari zilizokuwa zikitolewa na uongozi wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), wakati wa mkutano huo, jijini leo. Uongozi wa shirika hilo, ulikuwa ukielezea pamoja na mambo mengine, kazi, majukumu, mafanikio na malengo ya shirika hilo, katika kuihudumia jamii ndani ya nchi na Kimataifa.
Meneja Masoko wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), David George, akifafanua jambo kwa waandishi wa habari, wakati wa mkutano huo. Uongozi wa Shirika hilo, ulikuwa ukizungumza nao, kuelezea pamoja na mambo mengine, kazi, majukumu, mafanikio na malengo ya shirika hilo, Dar es Salaam leo. Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano cha shirika, Elia Madules na kulia ni Kaimu Meneja Huduma za Barua, Jason Kalile. 
Meneja Masoko wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), David George, akifafanua jambo kwa waandishi wa habari, katika mkutano huo, Dar es Salaam leo. Katikati ni Kaimu Meneja Huduma za Barua, Jason Kalile na kulia ni Ofisa wa Idara ya Habari, Maelezo, Frank Mvungi. 
Baadhi ya waandishi wa habari, wakiwa katika mkutano huo na uongozi wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), jijini leo. Kushoto ni Ofisa Uhusiano Mwandamizi wa shirika, Joseph Ngowi.
Kaimu Meneja Huduma za Barua wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Jason Kalile, akizungumza katika mkutano huo. Katikati ni Meneja Masoko wa Shirika hilo, David George na kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano cha shirika hilo, Elia Madules.
Meneja Masoko wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), David George, akizungumza katika mkutano huo, ambao uongozi wa shirika hilo, ulikuwa ukielezea pamoja na mambo mengine, kazi, majukumu, mafanikio na malengo ya shirika hilo, Dar es Salaam leo. Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano cha shirika, Elia Madules.
Waandishi wa habari, wakisikiliza maelezo yaliyokuwa yakitolewa na uongozi wa Shirika hilo la Posta Tanzania (TPC), wakati wa mkutano huo, jijini leo. Uongozi wa shirika hilo, ulikuwa ukielezea pamoja na mambo mengine, kazi, majukumu, mafanikio na malengo ya shirika hilo, katika kuihudumia jamii ndani ya nchi na Kimataifa.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano cha Shirika la Posta Tanzania (TPC), Elia Madules, akifafanua jambo kwa waandishi wa Habari, wakati uongozi wa shirika hilo, ulipokuwa ukizungumza nao, kuelezea pamoja na mambo mengine, kazi, majukumu, mafanikio na malengo ya shirika hilo, Dar es Salaam leo. Katikati ni Meneja Masoko wa shirika, David George na kulia ni Kaimu Meneja Huduma za Barua, Jason Kalile.
 


Na Frank Mvungi- Maelezo

Shirika la Posta Tanzania linatarajia kuanza kutoa huduma zake kwa wananchi kwa kutumia mfumo wa anuani za Makazi na Misimbo ya Posta kabla ya Mwisho wa Mwaka huu.

Hayo yamesemwa na  Meneja Masoko wa Shirika hilo Bw. David George wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam.

Akifafanua David  amesema kuwa kwa kuzingatia mpango kazi wake shirika hilo limedhamiria kufikia mwakani nusu ya Mikoa ya Tanzania Bara na Visiwani iwe imefikiwa na huduma ya anuani za Makazi na Msimbo wa posta.


Aidha David amesema kuwa huduma hiyo tayari imeanza kutolewa katika Mikoa ya Arusha  ambapo imehusisha kata 8, Dodoma kata 8 na Dar es salaam  hadi kufika June 2014 kata 27 zitakuwa zimefikiwa ambapo lengo kuu ni kuboresha huduma  na kufikisha barua pamoja na vifurushi katika makazi ya wateja kwa wakati.

Pia David alieleza kuwa Shirika hilo lina mpango kabambe wa kuleta mabadiliko makubwa katika uendeshaji na utoaji huduma za Posta nchini ili kunufaika na fursa zinazoletwa na mabadiliko ya teknolojia,kuboresha huduma,kukidhi mahitaji ya soko na kukabiliana na ushindani.


Akifafanua Bw. David amesema lengo ni na kuongeza tija kwa kutoa huduma zenye viwango vya kimataifa.


Shirika la Posta Tanzania linatekeleza mpango wa miaka 10  (2014-2023) unaozingatia juhudi kubwa zinazofanywa na Serikali kupitia utekelezaji wa sera na mipango mbalimbali ikiwa ni pamoja na Dira ya maendeleo ya Taifa 2025, Mpango wa Matokeo wakubwa sasa,sera ya posta 2003,Mkakati wa kukuza uchumi na kupunguza umasikini (MKUKUTA), Mpango wa kurasimisha rasilimali za biashara za wanyonge (MKURABITA), Mfuko wa Taifa wa anuani za Makazi na Sera ya Taifa ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA)

No comments:

Post a Comment