* Viongozi wa Chadema wabanwa kwa kuficha Mkataba wa Malipo ya Mnara wa Vodacom
Wananchi wakiwa mpakani mwa Mkoa wa Manyara na na Singida wakati wa
mapokezi ya Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana alipokuwa akianza
ziara Mkoa wa Manyara.
Kinana akiwa na Sumaye huku wakiwa wamezingirwa na vijana wa kabila la Wabarbaig walipowasili katika Kijiji cha Mahu, Hanang.
|
Wasichana wa kabila la Wabarbaig, wakishiriki katika mapokezi ya Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahaman Kinana katika Kijiji cha Mwahu, Hanang.
|
Wananchi wakisikiliza kwa makini wakati Kinana akihutubia mjini Rndasak, wilayani Hanang.
|
.Kinana na Nape wakimhoji vizuri Mwenyekiti wa Chadema wa Wilaya ya
Hanang, Augustino Mayumba aeleze alikopeleka hati ya mkataba wa mnara wa
simu wa Vodacom uliowekwa katika Kijiji cha Basouto ambao alishiriki
kutia saini ambapo hadi sasa malipo ya fedha hizo haijulikani nani
analipwa.
Hatua hiyo ya kumhoji ilifikiwa baada Kiongozi huyo kuuliza swali kwenye
mkutano wa hadhara wa CCM uliofanyika kwenye Kijiji cha Basouto kuwa
viongozi wa CCM wanakula fedha za malipo ya mnara huo uliowekwa eneo la
soko. Kinana alimtaka Mayumba aeleze mkataba huo ameuweka wapi. Licha ya
kiongozi huyo wa Chadema kukiri kushiriki kusaini mkataba huo lakini
alishindwa kueleza kwa kusema kuwa na yeye hajui mkataba huo ulipo,
jambo ambalo liliwafanya wananchi kuanza kumzomea. Kinana aliwataka
wananchi na serikali kumbana Mayumba hadi aeleze alipouweka mkataba
iliserikali ya Kijiji iwe inapata malipo hayo.
Sumaye ambaye pia aliwahi kuwa mbunge wa Jimbo la Hanang, akihutubia katika moja ya mikutano aliyoifanya Kinana wilayani Hanang. |
Kinana akishiriki kusomba mawe kwa ajili ya kujengea sakafu jengo la
CCM katika Kata ya Qaloda, wilayani Hanang. PICHA ZOTE NA KAMANDA WA
MATUKIO BLOG
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akihutubia katika mkutano wa hadhara uliofanyika mjini Katesh, Hanang. |
Mmoja wa wanachama lukuki walioambua kuachana na chama hicho na kujiunga na CCM akionesha kadi ya Cahdema kabla ya kukabidhiwa kadi ya CCM katika mkutano wa hadhara mjini Katesh, Hanang. |
Kinana na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye wakisaidia kupaua katika jengo la maabara la Shule ya Sekondari ya Mwahu walipoanza zira wilayani Hanang, Mkoa wa Manyara. |
Kinana akuhutubia katika Kata ya Basouto wilayani Hanang, Manyara. |
Wanamichezo wakimshukuru Mbunge wa Jimbo la Hanang, Dk. Mary Nagu na Kinana baada ya kukabidhiwa zawadi ya mipira na jezi wakati wa mkutano wa hadhara mjini Katesh, Hanang. |
Msichana wa kibarbaig akicheza ngoma wakati wamapokezi ya Kinana wilayani Hanang
No comments:
Post a Comment