Tuesday, May 20, 2014
Mwaka mmoja wa Benki ya TWB Dodoma wajasiriamali wanufaika
Mkurugenzi wa Benki ya Wanawake Tanzania (TWB), Margareth Chacha akifafanua jambo, wakati alipokua akizungumza na wajasiriali wa Mkoa wa Dodoma, alipofika kuona maendeleo yao na namna wanavyoshirikiana na Maofisa wa benki hiyo, waliopo mkoani hapo.
Wajasiriamali wa kada mbalimbali wakimfuatilia kwa makini hotuba ya Mkurugenzi wa Benki ya Wanawake Tanzania (TWB), Margareth Chacha, wakati akizungumza nao, aliyetembelea Dodoma ili kuona maendeleo yao, kibiashara na namna wanavyokuza mitaji kutokana na mikopo wanayopata toka benki hiyo.
Mkurugenzi wa Benki ya Wanawake Tanzania (TWB), Margareth Chacha akiwa katika pozi la picha ya pamoja na Mwenyikiti wa Kikundi cha Wajasiriamali chenye watu 40, Greace Kimario (kulia), tawi la Rusha Roho na kushoto ni Katibu wa tawi la Ipagala, lenye watu 50, Neema Ally, mara baada yakumaliza kuwapongeza kutokana na mwenendo mzuri wa marejesho ya mikopo huku kila mmoja wao, akinufaika kati ya wakopaji 3000 waliopo Dodoma.
Wajasiriamali wa kada mbalimbali wakimfuatilia kwa makini hotuba ya Mkurugenzi wa Benki ya Wanawake Tanzania (TWB), Margareth Chacha, wakati akizungumza nao, aliyetembelea Dodoma ili kuona maendeleo yao, kibiashara na namna wanavyokuza mitaji kutokana na mikopo wanayopata toka benki hiyo.
Na John Banda, Dodma
WAJASIRIAMALI mkoani hapa wametakiwa kuandika majina yao kwenya hati za mali wanazomiliki ili kuepuka hali ngumu ya kiuchumi ambayo imekuwa ikiwakumba watu wengi kipindi cha uzeeni.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Benki ya wanawake nchini (TWB), Margareth Chacha alipokuwa akizungumza na wajasiriamali wa Mkoa wa Dodoma alipofika kutaka kujua namna mikopo inayotolewa na Benki hiyo inavyowakwamua kiuchumi.
Mkurugenzi huyo alisema watanzania wengi wamekuwa katika wakati mgumu kimaisha katika maisha ya uzeeni kutokana na kutojitambua wakati bado wangali na nguvu za kutafuta mali na kuzitunza na wenzi wao wakati umiliki ukiwa wao wenyewe.
Alisema wajasiriamali wengi hasa wanawake wamekuwa wakiandika majina ya waume zao na watoto kwenye hati na stakabadhi za manunuzi hali ambayo inachangia wengi wao kukosa au kuchelewa kupata mikopo kutokana na hatua ndefu ya ushawishi ili hati hizo ziweze kutoka kwa walioandikwa majina yao.
‘’Sasa ukute mwanaume muelewa umuombe akupe hiyo hati ukakopee lakinikama siyo umekwama, pia kuandika majina ya watoto siyo mbaya lakini akikua anaondoka je wewe uzeeni utaishije, sasa hakikisha uanajiandaa vya kutosha kwa kutumia akili si nguvu na midomo’’, alisema.
Aidha Margareth alisema Benki hiyo imekuja na bidhaa mpya ijulikanayo kwa jina la mikopo ya maendeleo kwa ajili ya kuwanufaisha wajasiriamali ikiwemo kuwajengea nyumba kwenye viwanja wanavyomiliki na kutakiwa kulipa kidogokidogo, kuwanunulia bajaj, bodaboda, pik up, mashine za kukamua alizeti na viwanja.
Baadhi ya wajasiriamali hao Neema Ally na Greace Kimaro walimpongeza Murugenzi huyo kwa kuwajali na kufika kutaka kujua maendeleo yao yanayotokana na Mikopo wanayopewa katika benki hiyo ya TWB ambapo pia wameyajua mengi ambayo hawakuyajua kabla ikiwemo kulipa mkopo wa kilimo mara baada ya mavuno.
Tawi la Benki ya wanawake Tanzania (TWB), lina mwaka mmoja sasa tangu lifunguliwe mkoani hapa ambapo mpaka sasa lina jumla ya wanachama 3000 ambao wameshanufaika na mikopo inayotolewa kwa masharti nafuu huku ikitozwa liba ndogo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment