TANGAZO


Friday, May 23, 2014

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mbeya, Dk. Mary Mwanjelwa, akabidhi msaada wa mashuka 150, waathirika wa mafuriko wilayani Kyela

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mbeya, Dk. Mary Mwanjelwa, akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Mpunguti, huku akiwa amepiga magoti, Wilaya ya Kyela mkoani Mbeya, alipoenda kuwapa pole ya mafuriko na kukabidhi mashuka 150 katika Vijiji vya Mpunguti na Nyerere wilayani humo jana.
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mbeya, Dk. Mary Mwanjelwa (kushoto), akikabidhi mashuka kwa Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Mpunguti, wilayani Kyela jana, alipotembelea waathirika wa mafuriko wilayani humo na kutoa mashuka 150 katika Vijiji vya Mpunguti na Nyerere.
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mbeya, Dk. Mary Mwanjelwa, akipewa mkono wa shukrani na Mzee Lington Mwakatundu wa Kijiji cha Nyerere, Kata ya Bujonde, wilayani Kyela jana, alipotembelea waathirika wa mafuriko wilayani humo, na kutoa mashuka 150 katika Vijiji vya Mpunguti na Nyerere.
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mbeya, Dk. Mary Mwanjelwa (mbele), akivuka daraja la mianzi katika Kijiji cha Mpunguti wilayani Kyela jana,  alipotembelea waathirika wa mafuriko wilayani humo, na kutoa mashuka 150 katika Vijiji vya Mpunguti na Nyerere. (Picha zote na mpigapicha wetu).

No comments:

Post a Comment